Mwakyembe akutana na Diamond, wafanya mazungumzo


Waziri wa Utamaduni sanaa na michezo Dk,Harrison Mwakyembe leo Jumanne Machi 27,2018 amekutana na mwanamuziki Nassibu Abdul 'Diamond Plutnumz jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini,Lorietha Laulence imesema lengo la kukutana kwa wawili hao ni kulejesha maelewano kwenye tasnia ya muziki kufuatia hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo kufungia baadhi ya nyimbo zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Imeeleza kuwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Wizara hiyo na kuchukua zaidi ya saa tatu,kiliudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Juliana Shonza,katibu mtendaji wa Balaza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mwingereza.

Wengine ni Katibu mtendaji wa Bodi ya filamu Tanzania,Joyce Fisoo huku Diamond akifuatana na mameneja wake wa tatu Sallam Sharaf,Hamis Taletale na Said Fela.

Taharifa hiyo inaeleza mazungumzo hayo,Diamond alimhakikishia Dk Mwakyembe kushirikiana kwa karibu na Shonza na uongozi mzima wa wizara katika kusimamia maadili ya kazi za sanaa na kuwa mfano bora wa wasanii nchini katika kulinda utamaduni wa Tanzania.

Kwa upande wa Dk Mwakyembe amesisitiza kuwa Serikali haina ugomvi wowote na wasanii nchi bali inatatizo na mmomonyoko wa maadili,kwamba kila msanii ana wajibu kulinda maadili ambayo ni sehemu ya utamaduni wa nchi.

'Mwakyembe alikumbushia kauli ya Mwalimu Julius Nyerere baada ya Uhuru kwamba Taifa lisilo na utamaduni wake ni sawa na Taifa mfu na Watanzania kamwe tusigeuke Taifa mfu" inaeleza taharifa hiyo ikimnukuu Dk Mwakyembe.

Waziri huyo ameagiza watendaji wa wizara na taasisi zake ikiwemo Basata, bodi ya filamu na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kukutana na makundi ya wasanii wa muziki kwa lengo la kuelimisha kuhusu taratibu za kuwasiliana na mamlaka husika za sanaa.

"Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yanafanywa kwa mujibu wa sheria na si wa utashi binasfi wa kiongozi wa wizara,hivyo basi ieleweke kwamba hatua zilizochukuliwa Shonza hivi karibuni zilikuwa kwa mujibu wa sheria za nchi"amesema Dk Mwakyembe.

Kwa upande wake Shonza amesisitiza umuhimu wa wasanii kufuata utaratibu kwa kuwasilisha kazi zao mapema kwenye mamlaka husika ili kuepusha matatizo baadae.

Lorietha Laurence Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo. 27/3/2018.
Chanzo:Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako