Mrundi Simba Afichua Mbinu Za Ubingwa


Vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kwa kasi, Simba na Yanga ndizo timu ambazo zinatajwa kuwa na nguvu ya kupigania ubingwa huo ambapo zimesalia mechi chache kabla ya msimu wa 2017/18 kukamilika.

Licha ya kuwa Azam FC nayo ina nafasi lakini wababe hao wawili ambao wanashika nafasi mbili za juu kwenye msimamo ndiyo wanaopewa nafasi kubwa ya kufanya kweli kutokana na kasi yao pamoja na kasi yao ya kufunga mabao ilivyo nzuri.

Wakati hali ikiwa hivyo, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba, Masoud Djuma amefunguka kuwa watahakikisha wanapambana kufanikisha wanafanya vizuri katika michezo 10 iliyosalia ili kupata pointi zitakazowawezesha kupata ubingwa.

Simba wanaongoza msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 46 wakiwa wamesaliwa na michezo 10, Yanga wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 46 pia lakini wamezidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, pia wana michezo tisa iliyosalia.

Baadhi ya michezo ambayo bado Simba italazimika kuhakikisha inapata pointi tatu ni dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, Njombe Mji ya Njombe, Majimaji ya Ruvuma, Lipuli ya Iringa na Singida United ya Singida.

Djuma ambaye ni raia wa Burundi amesema wanahitaji kuelekeza nguvu kubwa kwa ajili ya michezo hiyo hasa ile ambayo watacheza nje ya Dar es Salaam kwa kuwa ndiyo itakuwa imebeba ubingwa kutokana na ugumu ambao watakutana nao kuliko ile ambayo watacheza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Amesema kuwa michezo ya mikoani ni migumu na huko wanatakiwa kuendelea kuongeza nguvu kwa kuwa mara nyingi mazingira yamekuwa yakiwaangusha.

Kocha huyo amabye ni mzuri katika kuzungumza na kujieleza katika lugha ya Kiswahili ameongeza kuwa pointi za mikoani ni ngumu lakini wachezaji wake wako fiti na watapambana kuhakikisha wanashinda.
Chanzo:Shutikali
MaoniMaoni Yako