Thursday, March 29, 2018

Mkwasa mambo safi TFF , aanza kulipwa deni lake

TagsKocha wa zamani wa Taifa Stars na Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema wamekubaliana na TFF kuanza kulipwa taratibu deni lake analodai.
Mkwasa aliondoka Stars akiwa hajalipwa fedha zake za mishahara wake wakati akifundisha timu hiyo, wakati Shirikisho hilo likiwa chini ya utawala wa Rais Jamal Malinzi.
Kupitia kipindi cha Michezo cha Radio EFM, Mkwasa amesema wameshakubaliana kuanza kulipana taratibu mpaka pale deni litakapokamilika, kwa sababu hata yeye ni kiongozi na anakumbana na madeni mbalimbali ndani ya wadhifa alionao Yanga.
Mkwasa alianza kuifundisha Stars baada ya kuipokea kutoka kwa Mdachi, Mart Nooij, aliyefungashiwa virago kuinoa timu hiyo Julai 21 2015.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz