Mkwasa atajwa AFC Leopards


Nairobi, Kenya. Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, Dennis Kitambi ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwania nafasi za kuifundisha AFC Leopards ya Kenya.
Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Kenya, AFC Leopards wanatafuta kocha mpya hasa kutoka nje ili kutimiza ndoto yao ya kupata ubingwa wa ligi hiyo baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu walipofanya hivyo 1998.
"Tumepokea CV za makocha mbalimbali na zimefikishwa kwa kamati yetu ya ufundi inayoongozwa na Jacob 'Ghost' Mulee na Simon Mulama kwa ajili ya kufanya mchujo. Bila ya ubishi atakuwa wakutoka nje," alisema katibu wa kamati hiyo Timothy Lilumbi.
"Vigezo vyetu vipo wazi kabisa, ni lazima aweze kuendana na mfumo wa sasa na ndiyo sababu ya kutaka kumtafuta sasa kabla ya kufika katikati ya mwaka huu, ila kwa sasa tunamfutilia kocha (Dennis Kitambi) ambaye kwa sasa yupo nje kwa masomo yake ya ukocha," alisema.
Pia, kocha wa zamani wa Taifa Stars na Yanga, Boniface Mkwasa ni miongoni mwa majina makubwa yaliyokuwa katika orodha hiyo.
Hata hivyo Mkwasa alipoulizwa kuhusu kutakiwa na AFC Leopards hakukubali wala kukataa zaidi ya kusema ni jambo la kusubiri.
“Sina taarifa za kutakiwa na AFC Leopards hivyo kama ni kweli, ngoja tusubiri tuone”alisema Mkwasa kwa kifupi.
MaoniMaoni Yako