Mkude kukaa nje ya uwanja wiki moja


Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude, imearifiwa anaweza akakosekana dimbani kwa takribani wiiki moja kufuatia kuumia juzi mazoezini.
Simba imekuwa ikifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam ambapo hivi sasa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji FC utakaopigwa Aprili 3 2018.
Kwa mujibu wa Daktari wa timu, Yassin Gembe, amesema Mkude anaweza akachukua wiki moja badala ya siku mbili au tatu zilizotajwa awali.
Mkude aliumia mguu wakati wa mwazoezi baada ya kukutana na Mzamiru Yassin wakati wakiwania mpira

Na Agape Patrick
Email agape@spoti.co.tz
Source: Saleh Jembe
MaoniMaoni Yako