Powered by Blogger.

Slider

Breaking

MICHEZO

HABARI

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

VIDEOS

» » Manara Afunguka Baada Ya Waarabu Kuitoa Simba Kombe La Shirikisho

Ofisa Habari wa Simba SC, Haji Manara amefunguka kuhusu matokeo ya timu yake pamoja na yale ya Yanga katika michuano ya kimataifa.
Timu hizo zote zimeshindwa kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa japokuwa Yanga itaendelea kushiriki katika hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Manara amesema sababu kubwa ni kukosa uzalendo kwa mashabiki wa timu zote ndio sababu inayosababisha timu za nyumbani kuharibu michezo yao kwani mashabiki wanawafanya wachezaji wacheze wakiwa  na mashaka.
Akiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara alisema haya: 
“Naona huko mitandaoni baadhi ya wanayanga wanataja sababu mojawapo ya timu za Bongo kutofanya vizuri uwanja wa nyumbani ni kukosa uzalendo kwa vilabu vyetu. Wanalosahau wao nililisema hadharani mapema na nikabezwa na viongozi wao..leo ndiyo mwaujua uzalendo?”
Hata hivyo, Manara amesema kwa sasa mashabiki wa Simba wataendelea kuwa wazalendo kwa timu ya taifa tu kwa kuandika:  “Nawaambia kwa sasa tutafanya zaid yenu..kama tudini tudani….uzalendo wetu utabaki kwa timu za Taifa tu”
Simba ilitolewa na Al-Masry ya Misri katika Kombe la Shirikisho licha ya timu hizo kupata matokeo ya sare katika mechi zote mbili, Waarabu hao wamesonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini, Yanga wao walitolewa na Township Rollers ya Botswana katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
CHANZO-SHUTI KALI.

Na Mwanahabari wetu: Richard Shiyo Barua pepe richard@spoti.co.tz

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post