Kuelekea kombe la dunia


KUELEKEA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2018 URUSI
Fainali za 12 za mashindano haya katika historia yalifanyika nchini Uhispania huku Argentina akisimama kama bingwa mtetezi.
Fainali hizo zina umaarufu wake mkubwa katika historia ya kombe hili adhimu katika tasnia ya mchezo wa soka kwa wanaume. Ndio michuano iliyoshuhudia ‘ pigo la penati ‘ kwa mara ya kwanza pia ufungwaji wa idadi kubwa ya magoli katika mechi moja.

PENATI
Kukubalika kwa matumizi ya adhabu kubwa ya penati kutumika katika michuano ya FIFA yalipitishwa mwaka 1976 na kihistoria mechi ya kwanza kutumia adhabu hiyo ilikuwa Januari 9,1977 katika mechi za kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia kati ya Morocco na Tunisia ambapo Tunisia waliwafunga Morocco kwa pigo hilo 1-0.
Penati ya kwanza kutumika katika michuano ya kombe la dunia kwa maana ya fainali rasmi ni za mwaka 1982 nchini Uhispania katika mchezo wa nusu fainali kati ya Ujerumani Magharibi na Ufaransa , Ujerumani wakishinda mchezo huo.

USHINDI MKUBWA
Fainali hizi pia kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwake mwaka 1930 zilishuhudia ufungwaji wa idadi kubwa ya magoli katika mechi moja.

Hungary aliweza kumtandika El Salvador 10-1 hatua ya makundi . Ushindi huo mkubwa uliweza kuvunja rekodi za fainali za mwaka 1954 pale Hungary tena alipoweza kuwachapa  Korea kusini 9-0 na fainali za mwaka 1974 pale ambapo Zaire ( sasa DRC ) alipopigwa 9-0 na Yugoslavia.

Mbali na rekodi hizo , fainali hizi za mwaka 1982 ndio ziliweza kuwapa fursa Cameroon na Algeria timu toka Afrika kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Italia waliibuka mabingwa wa fainali hizo ndani ya jiji la Madrid nchini Uhispania baada ya kumchapa Ujerumani Magharibi 3-1.

Asanteni
Nitaendelea kuwaletea dondoo za fainali zenye historia zake za kutukuka katika michuano hii kuelekea michuano ya 21 ya kombe hili la dunia zitakazofanyika nchini Urusi.

Source: @ Samuel Samuel
2018
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

MaoniMaoni Yako