Kuelekea kombe la dunia Urusi waamuzi England wapigwa stop

Wakati ikiwa imesalia miezi michache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi, jumla ya Waamuzi 36 wametangazwa kuchezesha mashindani hayo.
Gumzo kubwa orodha hiyo ni kukosekana kwa Waamuzi kutoka taifa la England na sababu inayotajwa ni kushindwa kumudu kuchezesha vizuri.
Inaelezwa kuwa England imekuwa na Marefa ambao wamekuwa wakiboronga kuchezesha na hicho kinawezekana kikawa kigezo kikubwa cha kushindwa kuteuliwa kuhusika kwenye Kombe la Dunia mwaka huu. 
Mbali na England, FIFA pia hawajatoa hata Mwamuzi mmoja kutoka Mataifa ya nchi za Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini.
Uamuzi huo wa FIFA umewafanya wadu wa soka kila mmoja kuzungumzia lake baada ya uteuzi huo kufanyika leo.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz