Kamati Ya Rufaa Ya TFF Yamuita Wambura.


NA ALEXANDER VICTOR

Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF imemuita aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ambaye alifungiwa maisha kujihusisha na soka kwenda kujitetea kuhusu rufaa aliyoikata.


Ikumbukwe kuwa mchana wa Machi 15, 2018 Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), imemfungia maisha kutojihusisha na shughuli za soka Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura.

Inadaiwa kuwa Wambura amefungiwa kutokana na kupokea fedha zisizo halali kiasi cha Shilingi milioni 84, pamoja kughushi nyaraka za malipo, na kula njama kulipwa fedha na waliokua viongozi wa TFF Jamal Malinzi na Selestin Mwesigwa.
MaoniMaoni Yako