Jina la ngoma mpya ya Roma Mkatoliki lazua gumzo, Mkewe ahofia kumpoteza


Picha inayohusiana
Kila mdau wa muziki nchini Tanzania kwa sasa anahamu ya kusubiri wimbo mpya wa rapa Roma Mkatoliki hii baada ya mkali huyo wa Hip Hop kupitia katika kipindi kigumu cha kufungiwa wimbo wake na yeye mwenyewe kupigwa marufuku ya kutojihusisha na muziki.
Roma Mkatoliki na Mkewe
Sasa habari nzuri ni kwamba jina la wimbo wake mpya ambao unatarajiwa kuachiwa limeshavuja na sio lingine ni  “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU” jina ambalo limevujishwa na mkewe.
Mkewe na Roma Mkatoliki, Nancy amesema anajua magumu anayopitia mumewe na anawaza endapo ataachia wimbo huo wa “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU” maisha yake yatakuwaje? kwani ugumu wa mashairi yaliyomo kwenye wimbo huo yanamtia hofu.
Dah Nawazaa Sijui Baba Ataimba Nini Sasa Round hii! Kila Angle Wanakukazia!! Nawaza Ukiachia Ile “NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU.“ameandika Mke wa Roma kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo, Nancy amemshauri Roma asiuachie wimbo huo kwani bado anampenda na anahofia kumpoteza.
Lakini Daaah Bora Ukae Kimya Tu!! Bado Nakuhitaji Mume Wangu!! Nways Tutege Sikio Tu!!“ameandika Nancy.
Kwa upande mwingine, Mashabiki na wadau wa muziki wametoa maoni yao ambapo kila mmoja ameonekana kumsapoti mkewe na Roma wengine wanataka wimbo huo utoke.
Alhamisi ya  Machi 29, 2018 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe alitangaza kumfutia adhabu ya kifungo cha miezi sita rapa Roma Mkatoliki alichopewa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Juliana Shonza.
Hakuna asiyefahamu makali ya ngoma za Roma Mkatoliki na wewe mdau wa muziki una lipi la kumshauri Roma Mkatoliki kwa jinsi unavyoona jina la wimbo huo?
MaoniMaoni Yako