HAJI MANARA: Kichuya ni Messi wa Bongo


Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya, ametajwa kuwa Messi wa Tanzania baada ya kuifungia Taifa Stars bao la pili dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kichuya alifunga bao hilo katika dakika ya 87 kufuatia kazi nzuri ya Mbwana Samatta aliyemtengenezea pasi na kumalizia kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililompita Mlinda Mlango wa Congo.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, aliandika kiufupi akimuelezea mchezaji huyo kuwa ni dhambi kumfananisha na Lionel Messi anayekipiga na FC. Barcelona halikadhalika timu ya taifa ya Argentina.
Manara amesema Kichuya anastahili kuwa Messi wa Tanzania kutokana na namna anavyojua kuuchezea mpira, amekuwa akifunga pia kuwatengenezea wenzie nafasi zingine za kufunga.
Na Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Source: Saleh Jembe
MaoniMaoni Yako