Diego Costa awaonya mashabiki wa Argentina kuhusu Messi(la pulga)


Mshambuliaji wa klabu ya Atletico de Madrid na timu ya taifa ya Spain, Diego Costa, amewaonya mashabiki wa timu ya taifa ya Argentina kuhusiana na nyota Lionel Messi.
Costa ameyasema hayo ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kuchezea kichapo cha jumla ya mabao 6-1 kutoka kwa Spain.
Costa ameeleza kuwa mashabiki wa taifa hilo hawapaswi kumsema Messi ambaye hakucheza jana, bali washukuru kuwa na mchezaji kama huyo ambaye ni msaaada mkubwa kwa Argentina.
Vilevile Costa anaamini Argentina bila Messi haiwezi ikafika popote, hivyo Wanaargentina wote wanapaswa kuwa watulivu na si kumuongelea Messi kwa ubaya.
Kumekuwa na malalamiko baadhi kutoka kwa mashabiki wa Argentina kuhusiana na Messi kutocheza mechi ya jana baada ya timu hiyo kupoteza kwa idadi hiyo kubwa ya mabao.
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
Source: saleh jembe
MaoniMaoni Yako