Dani lyanga anapiga misele DSM singida ikijiaandaa kuwavaa yanga

Wakati klabu ya Singida United ikijifua kwa mara ya mwisho leo kuelekea mchezo wa Kombe la Shikisho dhidi ya Yanga kesho Jumapili, mchezaji Daniel Lyanga ameonekana akiwa mitaa ya jiji la Dar es Salaam.
Lyanga ameonekana akiwa mitaa ya Kinondoni akibadilishana mawazo na washikaji zake wakati klabu yake ikiwa inajiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Yanga kesho. 

Taarifa zilizotoka hivi karibuni zilieleza kuwa Lyanga amefungiwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuitumikia Singida United kwa muda wa miezi 6 kutokana na kusaini mkataba na timu hiyo wakati huohuo alikuwa ana mkataba mwingine na Fanja SC ya Oman.
Licha ya ujio wa taarifa hizo, Uongozi wa Singida United ulikanusha vikali uwepo wa taarifa hiyo ukieleza si kweli wala hajafungiwa.

Uongozi huo kupitia Mkurugenzi wa timu, Festo Sanga, ulisema kuwa kilichotokea ni kuchelewa kwa ITC ambayo bado haijatumwa mpaka sasa kufuatia dirisha dogo la usajili Ligi Kuu Bara kufungwa, na hivyo itabidi wasubiri mpaka Julai pale itakapowasili.
Lyanga hajaonekana kwenye mechi za mashindano rasmi yanayosimamiwa na TFF ('Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la TFF ‘Azam Sports Federation Cup’), mara ya mwisho kuonekana akicheza mechi za Singida United ilikuwa kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2018 visiwani Zanzibar.

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako