Azam yawatumia salam mtibwa kabla ya mechi ya leo

Kazi ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports inasubiriwa kwa hamu kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam wakati Azam FC ikiikaribisha Mtibwa Sugar.
Tayari wageni wameonekana kujiamini na kusisitiza wako tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Lakini Azam FC nao wamesisitiza hawatakuwa na utani na mtu na wanachotaka ni kuituliza Mtibwa Sugar na kuivurumisha nje ya michuano hiyo.
Kocha Msaidizi wa Azam, Idd Cheche amesema wamejipanga vizuri tena sana.
“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika mechi hii, kwani kwa sasa FA ndiyo michuano pekee ambayo tunaitegemea katika harakati zetu za kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa.
“Kwa hiyo, tutapambana kufa au kupona ili tuweze kupata ushindi katika mechi hiyo,” alisema Cheche.
Mechi nyingine ya robo fainali ya FA itakayochezwa leo itaikutanisha Prisons dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wakati Yanga itakuwa mgeni wa Singida United kesho kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.
Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako