Azam Yajipanga Kuimaliza Mtibwa Sugar


Klabu ya soka ya Azam FC imeweka wazi kuwa itaingia na moto wake wote kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex.
“Mchezo huu ni muhimu sana kwetu lazima tuwashe moto wetu wote mana mshindi atasonga mbele zaidi kwenye nusu fainali na ukichukua kombe utapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika'', amesema Idd Cheche ambaye ni kocha msaidizi.

Azam FC na Mtibwa zimeonekana kuwa na rekodi sawa kwenye michuano hiyo msimu huu ambapo Azam FC katika hatua za awali ilizifunga Area C United (4-0), Shupavu (5-0) huku Mtibwa Sugar nayo ikizifunga Villa Squad ya Kinondoni kwa mabao 2-1.
Katika hatua ya 16 bora Mtibwa iliitoa timu ya Buseresere, ambao ni mabingwa wa Mkoa wa Geita. Kwa upande wao Azam FC waliitoa KMC ya Kinondoni ambayo imepanda kucheza ligi kuu kuanzia msimu ujao.

Msimu huu tayari timu hizo zilikutana kwenye ligi na ikashuhudiwa zikitoka sare ya bao 1-1, bao la Azam FC lilifungwa na winga Enock Atta huku lile la Mtibwa Sugar likifungwa na Kelvin Sabato ‘Kiduku’ 
Source: Udaku Specially
MaoniMaoni Yako