Wasiooa Wakwamwa Kwa Waliooa, Wanyooshwa 3-0, Zachapwa Kavukavu

1 month ago 221

Wasiooa Wakwamwa Kwa Waliooa, Wanyooshwa 3-0, Zachapwa Kavukavu

TIMU ya Wasioa wameshindwa kufuta uteja mbele ya Walioa katika mchezo maalumu uliopigwa Ijumaa Julai 30, 2021 kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Dk Reginald Mengi, Dar huku wachezaji nguli wa Wasioa wakitaka kuzichapa kavukavu wenyewe kwa wenyewe.

 

Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi wakiwemo wadhamini wa mchezo huo kutoka Smart Gin, Creative Bee ambao umemalizika kwa Wasioa kukubali kichapo cha mabao 3-0.
Hii ni mara ya pili kwa Wasioa kukubali kichapo katika mchezo huo ambao umekuwa maalum kwa Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Group huku ukishirikisha washirika wake mbalimbali.


 

Wachezaji wa Wasioa walianza kuwa watata baada ya mwamuzi kutoa faulo ambayo ilipelekea kushikana kati ya mchezaji wa Walioa, nahodha Philip Nkini na beki wa Wasio, Marco Mzumbe kabla ya kuamuliwa na wachezaji wengine akiwemo Musa Mateja aliyeamua kujipa ukocha baada ya timu yake kuona inalekea kubaya lakini hakuweza kusaidia chochote.
Lakini hali ya kutoelewana kwa wachezaji wa Wasioa iliendelea kuwa kubwa baada ya kwenda mapumziko ambapo mshambuliaji mwenye maneno mengi, Hussein Msoleka ‘Mpemba wa Dar’ kutaka kuzichapa na shabiki wa timu yake Kenny kisa tu kuambia aache kupoteza mpira ovyo lakini waliwahi kuamuliwa.
Walioa wameibuka na ushindi huo wa mabao 3-0 licha ya timu ya Walioa kumkosa nyota wake mkubwa Saleh Jembe ambaye hakuwepo kwenye mchezo huo uliodhamiwa na Smart Gin, Creative Bee, Championi, Spoti Xtra, Wezesha Mzawa, +255 Global Radio, Global Tv Online na Tukuyu Spring Water.