Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 27.07.2021

1 month ago 214

Je Paul Pogba ataepuka shoka Man United msimu huu?

CHANZO CHA P IMAGES

Juventus wamemueleza Cristiano Ronaldo, 36 kwamba wanatarajia asalie klabuni hapo msimu huu. Mshambuliaji huyo mreno, amekuwa akihusishwa kutaka kutimka wakati huu ambapo mkataba wake ukisalia na mwaka mmoja kuisha. (Sky Sports)

Juventus wameonyesha nia ya kumuuza Aaron Ramsey, 30 msimu huu, kiungo huyo wa Wales, anaonekana kama mzigo kwa Klabu kwa sababu ya mshahara wake mkubwa. (Gazzetta dello Sport, via Mail. 

Manchester United watamsajili beki wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane kwa mkataba wa miaka minne na uwezekano wa kuongeza mwaka mwingine mmoja, lakini haifahamiki hasa ni lini beki huyo mwenye umri wa miaka 28 atafanyiwa vipimo vya afya kwa sababu ya masharti ya Corona ya kukaa ndani. (Athletic - subscription required)

Newcastle wanapambana kukamilisha usajili wa beki wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, Axel Tuanzebe, 23, kutoka Manchester United. (Telegraph)

Ben White, 23 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Jumatano Arsenal huku uhamisho wa mlinzi huyo wa England wa £50m ulisharidhiwa na Brighton tangu wiki iliyopita. (Sky Sports)

LUKAKU

CHANZO CHA P


ROMELU LUKAKU, 28, ANAFURAHA INTER MILAN NA MSHAMBULIAJI HUYO WA UBELGIJI, HANA MPANGO WA KUONDOKA KLABUNI HAPO MSIMU HUU, LICHA YA CHELSEA KUONYESHA NIA YA KUMTAKA (EXPRESS)

Tottenham wanaongeza nguvu ya kujaribu kumnasa beki wa kati wa Atalanta na Argentina Cristian Romero, 23, kwa ada ya £40m. (Telegraph)

Ofa ya Aston Villa ya kumsajili winga wa Bayer Leverkusen Mjamaica Leon Bailey imeanza kuwa ngumu kufuatia vilabu vya Leicester, Everton, Wolves na Southampton kuonyesha nia ya kumtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, anayepatikana kwa ada ya £30m. (90min)

BARCELONA

CHANZO CHA PICHA,

Barcelona hawajapokea mpaka sasa maombi yoyote ya usajili kwa ajili ya mshambuliaji wao mfaransa Antoine Griezmann, 30. (Marca - in Spanish)

Xherdan Shaqiri, 29, anajiandaa kutimka Liverpool msimu huu, huku Napoli na Lazio ni baadhi ya vilabu vilivyoonyesha nia ya kutaka kumsajili winga huyo wa Switzerland. (Goal)

Arsenal wanafikiria kumsajili winga wa kireno Matchoi Djalo, 18, kutoka Pacos de Ferreira anayepatikana kwa ada ya £1m. (Sun)

West Ham wameonyesha nia ya kumsajili mlinzi wa Denmark Jens Styger Larsen, 30, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Udinese na anaweza kugharimu £4.2m. (Football.London)

austria

CHANZO S

Mshambuliaji wa zamani wa West Ham na Stoke Marko Arnautovic, 32, atawasili Italia wiki hii - Muaustria huyo anakamilisha uhamisho wake kutoka Shanghai Port ya China kwenda Bologna. (Corriere dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa Newcastle Mjapan Yoshinori Muto, 29, yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na Aris Salonika ya Ugiriki baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo kwenye klabu ya Hispania ya Eibar. (Newcastle Chronicle)

Timu ya League One ya Wycombe wako katika mazungumzo mazuri ya kumsajili mshambuliaji wa Wales Sam Vokes, 31, kutoka Stoke ya Championship. (Football Insider)

Source BBC Swahili