Testesi za usajili Barani Africa

1 month ago 210


✍️ Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amewasilisha barua kwa uongozi wa klabu hiyo ya kuomba kusitisha mkataba wake ili kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, huku kukiwa na tetesi Mk14 anaweza kujiunga na APR ya kwao Rwanda.

✍️ Baada ya kuachana na Horoya H. E. Makambo yupo Kwenye mazungumzo na waajili wake wa zamani klabu ya Yang, Makambo huenda akasaini mkataba wa miaka 2 wa kuitumikia klabu hiyo.

✍️ Klabu ya yanga sc ipo kwenye mazungumzo na Kiungo wa kimataifa wa Uganda @KhalidAucho mwenye umri wa miaka 27, awali kiungo huyonalikuwa anawindwa na Simba sc

✍️ RASMI: Mabingwa ligi kuu ya Guinean klabu ya Horoya AC 🇬🇳 imethibitisha kumsajili kiungo wa kimataifa wa Mali Issaka Samake mwenye umri wa miaka 26 na Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Pape Abdou Ndiaye mwenye umri wa 19 akitokea Stade Malien 🇲🇱 na ASC Jaraaf 🇸🇳

Pape na Samake wote wamesaini mkataba wa miaka 3 wa kuitumikia Horoya fc.

✍️    🇶🇦RASMI: Klabu ya @DuhailSC Ya nchini Qatar imethibitisha kumsajili kiungo wa kimataifa wa Tunisia 🇹🇳 Ferjani Sassi mwenye umri wa miaka 29 kwa mkataba wa miaka 3 akitokea Zamalek SC 🇪🇬 kwa usajili wa bure.