Simba bingwa tena wa FA, akimchapa Yanga

1 month ago 521

UWANJA wa Lake Tanganyika,  Kigoma katika fainali ya Kombe la Shirikisho, Simba imetwaa taji Lake mara mbili mfululizo baada ya msimu uliopita kufanya hivyo mbele ya Namungo FC ba leo ilikuwa mbele ya Yanga.


Ni Taddeo Lwanga alipachika bao la ushindi kipindi cha pili ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Ilikuwa ni pigo la kichwa akitumia mpira wa kona iliyopigwa na Luis Miquissone ambaye leo ilikuwa ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani.


Ni dakika ya 79 baada ya ngoma kuwa nzito dk 45 za mwanzo ambazo Yanga iliziyeyusha ikiwa pungufu ndani ya uwanja.


Ni Mukoko Tonombe raia wa Congo alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga kiwiko nahodha wa Simba John Bocco ilikuwa dk ya 43.


Simba inatangazwa kuwa bingwa wa Kombe la Shirikisho mbele ya mtani wake wa jadi, mwisho wa reli Kigoma.