Kesi ya Morrison na Yanga bado kidogo

1 month ago 257

Kesi ya Morrison na Yanga bado kidogo

BAADA ya mashabiki wa soka ndani na nje ya nchi kusubiri hatima ya kesi ya Yanga dhidi ya mchezaji Bernard Morrison ambayo ilikuwa inaunguruma leo kwenye Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) taarifa sasa imetoka.


Yanga kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii imethibitisha kuwa CAS imemaliza kulisikiliza kesi ya rufaa ya Klabu ya Yanga dhidi ya Bernard Morrison.


Yanga wamesema mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kuanzia sasa mpaka Agosti 24, 2021.


"Uongozi wa Yanga unawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki kuwa na subira, wakati huu ambapo Mahakama hiyo inaendelea kukamilisha uamuzi wake" wameandika Yanga


kesi pic 1

Kwa upande wao klabu ya Simba waliweka picha za Morrison na kuandika "Tunakupenda na tupo pamoja nawe wakati wote,"