Kagere atoa neno kusalia Simba msimu ujao

1 month ago 243

Kagere atoa neno kusalia Simba msimu ujao

Mshambuliaji wa Simba amefunguka kwamba katika kipindi ambacho amepitia wakati mgumu ndani ya Simba ni msimu huu ambao Simba ilichukua taji la nne kwa mfululizo.

Akizungumza na kituo cha Radio ya B&B ya kwao Rwanda Kagere amesema msimu uliomalizika ulikuwa na changamoto nyingi kwake ndani ya Simba huku akimshukuru Mungu.

"Namshukuru Mungu kwa kumaliza msimu huu tumeshinda mataji mawili katika msimu huu,binafsi nimepitia moja kati ya msimu mgumu tangu nifike Simba.

Aidha Kagere amesema kwamba licha ya magumu hayo aliyopitia ambayo hakuyaweka wazi ametamka kwamba siku chache zijazo atawashangaza wengi.

"Watu watulie nitawashangaza ndani ya siku chache kutoka sasa," amesema Kagere kwa kifupi ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa ligi mara mbili tangu atue Simba.

Msimu huu Kagere tangu atue kocha Didier Gomes raia wa Ufaransa ambaye aliwahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma wakiwa Rwanda mshambuliaji huyo amekuwa akikosa kuanza katika kikosi cha kwanza.

Kagere amemaliza msimu huu akiwa na mabao 13 ikiwa ndio idadi ndogo zaidi tangu atue Simba ambapo mara mbili akiwa mfungaji bora aliwahi kufunga idadi ya juu mabao 23 huku nyuma yake katika msimu mwingine akifunga mabao 22.