| Waafrika wang'ara tena Ulaya |
| Monday, 12 March 2012 12:39 |
|
| Wikiendi iliyopita imekuwa tena nzuri kwa wachezaji wenye asili ye Afrika kuonyesha cheche zao tena katika timu wanazochezea majuu. Mchango wao ulionekana kwa wengi wao kuzifumania nyavu na wengine kutoa msaada pasi za mwisho zilizosaidia kupata ushindi. Waafrika wafuatao wamefunga magoli wikiendi hii:
DIDIER DROGBA, CHELSEA (IVORY COAST)
Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Ivory Coast anayecheza Chelsea ya Uingereza wikiendi hii alifunga goli pekee liliwafanya Chelsea kuondoka na pointi 3 muhimu walipocheza dhidi ya Stoke City. Licha ya kuwa mchezaji wao mmoja alipewa kadi nyekundu tangu dakika ya 25, Stoke waliendelea kuwasumbua Chelsea kwa kuziba mapendo njia zote za viungo wa Chelsea mpaka dakika ya 68 Drogba alipufunga goli pekee akiunganisha pasi kutoka kwa Juan Mata. Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza ya ligi kwa kocha wa mpito Roberto Di Matteo baada ya kocha Villas boas kutimuliwa hivi karibuni kwa matokeo mabaya tangu aichukue timu hiyo.
|
|
|
| Waafrika wang'ara majuu wiki hili |
| Monday, 05 March 2012 11:43 |
|
| Wiki limeisha kwa wachezaji wenye asili ya Afrika kung'ara na klabu wanazozichezea ulaya. Hii imetokana na mchango wao aidha kwa kufunga magoli au kusaidia magoli yenyewe. SPOTI linakuletea wanasoka hao waliozifumania nyavu wiki iliyopita:
1. Seydou Keita
Mchezaji huyu mwenye asili ya Mali anayechezea Barcelona ya Hispania aliisaidia timu hiyo kwa kufunga goli mihimu katika
|
|
|
|
|
|
|