Ronaldinho: Hela kwake si kitu
Written by Mwandishi Spoti    Monday, 11 June 2012 08:29   

RONALDINHO Gaucho ni mwanasoka nyota wa Kibrazil ambaye amekuwa akicheza soka kama kiungo mshambuliaji na ni mtundu mtundu wa kuchezea mpira  na anavutia mno uwanjani.

Jina lake halisi ni Ronaldo de Assis Moreira aliamua kuitwa Ronaldinho kwa kufuata matamshi ya lugha ya Kireno na kujitofautisha na akina Ronaldo wengine ambao ni wengi huko Brazil, kama walivyo akiwa Massawe, Mushi huko Moshi ama akina Sanga huko Njombe, Iringa.

Gaucho ni jina lake la kimichezo ambalo linamtofautisha zaidi na akina Ronaldo wengine.

Kutokana na umahiri wake wa kucheza mpira katika sehemu ya kiungo na kushambulia amefunga magoli mengi katika klabu alizochezea na timu yake ya taifa.

Timu yake ya mwisho kuichezea ni Flamengo na akachaguliwa tena kuichezea Brazil inayotumia jezi za njano na bluu.

Kwa sasa ameachana na Flamengo, kwa madai kuwa ilikiuka mkataba wa kutomlipa mshahara wake.

Ni mmoja kati ya ya wachezaji mahiri wa soka duniani na aliwahi kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia mara mbili 2004 na 2005.

Alipata mafanikio makubwa katika uchezaji soka alipokuwa katika timu ya FC Barcelona kisha alihamia katika kikosi cha AC Milan.

Lakini katika miaka ya karibuni alipungua kiwango kitu kilichochangiwa na kuongezeka uzito, pengine ni kutokana na kustarehe baada ya kuwa fedha.

Ronaldinho ni mmoja kati ya wanasoka matajiri duniani aliyepata fedha kupitia uchezaji wake kwenye klabu kubwa duniani na kuingia mikataba minono na makampuni makubwa yaliyokuwa yakimlipa kwa matangazo.

Amekuwa akipata kiasi cha dola milioni 24 kwa mwaka.

Anaelezwa kuwa alikuwa akipata kiasi cha euro milioni 25 kwa mkataba wake wa miaka mitatu katika timu ya AC Milan ya Italia.

Anakadiriwa alikuwa akilipwa dola milioni 10 kwa mwaka kutokana na mshahara wakati alipokuwa Barcelona.

Ametengeza fedha nyingi kwa kuonekana katika matangazo ya kampuni za Nike na Pepsi. Anaaminika kuwa na utajiri wa dola milioni 90.

Ronaldinho kama watu wengi walio na fedha, naye si haba anajua kutumia kwa kuishi maisha ya kifahari kutokana na kuzichanga kwa kutumia kipaji chake cha soka.

Anamiliki nyumba kadhaa kwao Brazil na Hispania. Jumba lake la Hiapania ni bab kubwa na lina nafasi kubwa. Jumba hilo limepambwa likiwa na thamani za bei mbaya huku kwenye kuta zake likiwa na michoro ya gharama pia.

Anamiliki na kuendesha magari ya bei mbaya ya kifahari miongoni mwake ni Mercedes-Benz E-class na Mercedes-Benz CLS.

Si mtu wa wa kupenda kujibanabana, kwani amekuwa akisafiri kwa kutumia ndege ya kukodi anapokuwa na safari.

Kwa kuwa ni mtu anayefahamika na mwenye ushawishi kwa jamii anamiliki mfuko wa hisani kwa ajili ya kusaidia watu wengine, kuna wakati aligombana na kaka yake kwa kutumia fedha vibaya.

Ronaldinho alizaliwa kutoka katika familia ya tabaka la kati nchini Brazil.

Baba yake alikuwa akifanya kazi getini na alipatwa na mkosi wa kufiwa na baba yake wakati akiwa mdogo na umri wa miaka nane.

Katika familia yao amezaliwa pamoja na kaka yake na dada yake.

Amekuwa na mahusiano na wanawake wengi na anajulikana kwa kuwa mahusiano ya mwanamke wa Kifaransa wakati alipokuwa Barcelona.

Ana mtoto wa kiume aliyepata kutokana na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na dansa wa Kibrazil, Janaina Mendes.

Kwa kumbukumbu aliamua kumpatia mwanaye jina la marehemu baba yake.  Kwa sasa anadaiwa kuoa, awali alioana na na Milene Domingues lakini alitaliakiana naye.

Ronaldo anamiliki gari la bei mbaya aina ya Bugatti Veyron ambalo linasifika kwa kuwa na kasi. Gari hilo la mashindano limekuwa liteka nyoyo za watu wengi akiwemo Ronaldinho mwenyewe. Limekuwa na mvumo kama wa nyuki likiwa na uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kilometa 253 kwa saa na injini ya W16.  alilinunua gari hilo kwa dola milioni 1.8.

Anapokuwa nyumbani hupenda sana kuliendesha gari hilo ambalo nalo lina kazi kubwa ambalo hulitumia wakati wa kwenda mazoezini.

Ana gari Hummer H2, ambalo ni imara  lenye nguvu. Ni gari la ajabu wakati linapotokea ambalo humvutia mtu kuliangalia. Unaweza kusema kuwa haliendani na hadhi yake lakini ndiyo hivyo amelipenda. Ni moja kati ya magari yanapendwa na mastaa wa majuu mmoja wapo akiwa ni mcheza sinema za kibabe Arnold Alois Schwarzenegger.

Kutokana na kuwa na nguvu na kuwa na tairi kubwa, gari hili liweza kupita hata katika barabara mbaya.

Ronaldinho hajazubaa kuhusu kujenga na kumiliki nyumba ya maana. Ana nyumba kubwa na Hispania ya kifahari ambayo mbele yake kuna ufukwe na ina eneo kubwa na ametumia malioni ya dola kuitengeneza.

Nyumba hiyo ina vyumba vikubwa na mabafu, vyumba kwa ajili ya wageni na ukumbi mkubwa, Ina Chumba kikimbwa chenye madirisha makubwa ya vioo vinavyomwezesha mtu anakuwa ndani kuona madhari ya nje.

Eneo ilipo nyumba hiyo ni tulivu, wanayu wanafika hapo huweza kutuliza fikra zao na kujiona wako sehemu ya faragha.

Kuhusu samani zilizopo ndani yaani we acha tu, ni za nguvu na za bei mbaya pamoja na sakafu ya marumaru. Ina bwawa la kuogelea ambapo pembeni yake kuna taa za rangi ya bluu.

Kwenye bustani yake kumepandwa miti ya jamii ya mitende na majani. NI nyumba ambayo mtu akiwa nayo anaweza kujivuna na hasa akiwa na fedha huweza kujiona kama yuko kwenye paradiso fulani.

 

 

 

AddThis Social Bookmark Button

 
Kinda yupi kung'aa EURO 2012
Written by Mwandishi Spoti    Sunday, 03 June 2012 13:40   


ZIMEBAKI siku tano kabla ya fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya hazijaanza. Washabiki wa soka duniani kote watakuwa wanasubiri kuwaona wachezaji kama Xavi, Cristiano Ronaldo, Robin Van Persie na Zlatan Ibrahimovich wakifanya mambo makubwa.

Lakini kama ilivyo katika mashindano mengine yote hakukosi kuwa na staa mpya anayezaliwa kama ilivyokuwa kwa Enzo Scifo ambaye mpaka sasa anabaki kuwa mchezaji mdogo kuliko wote kucheza fainali hizo toka zianzishwe. Baadae waliibuka akina Maldini, Cristiano Ronaldo na Wyne Rooney

Makocha wa timu shiriki mwaka huu wamejaribu kujumuisha baadhi ya makinda katika vikosi vyao. Makinda hawa wana uwezo mkubwa na wanatarajia kufuata nyayo za akina Rooney na Maldini. Je makinda hao ni akina nani?


Jack Butland (England, 19 )

Alipopelekwa kwenda kucheza kwa mkopo katika timu ya daraja la tatu Cheltenham mwanzoni mwa msimu uliopita, Jack Butland hakuota hata kidogo kuwa angepanda ndege na kusafiri na England kwenda kushiriki fainali za mwaka huu.

Kuumia kwa golikipa namba tatu wa England John Ruudy kulimfanya kocha Hodgson kumwita kijana huyo ili kuchukua nafasi ya Ruudy.

Mashabiki wengi wa England watakuwa wanajiuliza Butland ni nani lakini golikipa huyu mwenye urefu wa sentimeta 193 sio mgeni kwa kocha wa timu ya vijana ya England stuart Pearce amabye alimpa nafasi mara sita katika timu hiyo ya vijana


Kostas Fortounis (Greece, 19)


Uwezo wa Fortounis ulionekana wakati alipoanza kuichezea Asteras Tripoli FC. Huko Juventus walivutiwa na uwezo wa kijana huyu na kutaka kumsajili kwa mkopo Januari 2011. Juventus wakashindwa kumchukua na mchezaji huyo akaamua kujiunga na Kaiserslautern FC ya Ujerumani.


Akiwa huko alionesha kiwango kikubwa licha ya timu yake kutofaanya vizuri katika ligi. Kiwango alichoonesha kilimshawishi kocha wa timu ya taifa ya Ugiriki kumpa nafasi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ubeligiji nafasi ambayo aliitumia vizuri na kumshawishi kocha wake kumjumuisha katika kikosi kitakachoshiriki fainali za mwaka huu.

 

Maxym Koval (Ukraine, 19)

Golikipa huyu alianza kuidakia timu ya Metalurh Zaporizhya akiwa na miaka 16 tu. Hii ni baada ya kipa chaguo la kwanza wa timu hiyo na chaguo la pili kuumia. Nafasi hiyo aliitumia vizuri na kuonesha kiwango kikubwa.

Kiwango alichokionesha wakati akiidakia timu yake dhidi ya Dynamo Kyiv kiliishawishi Dynamo Kiev kumsajili na toka hapo amekuwa akionesha kiwango kizuri anapopewa namba.

Kijana huyu alijumuishwa katika kikosi cha Ukraine kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi. Ni muda tu ndio utakaodhihirisha kiwango cha kinda huyu ambaye anawania namba na   Andriy Pyatov na Oleksandr Goryainov,

 

Jores Okore (Denmark, 19)

Beki huyu mzaliwa wa Ivory Cost alianza kuichezea timu yake kwa mara ya kwanza msimu uliopita. Tokea hapo Okore hakuangalia nyuma. Amekuwa chaguo la kwanza la timu ya Nordsjælland na kuweza kuisaidia timu hiyo kushinda kombe la ligi kuu ya Denmark kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo

Kiwango kizuri alichoonesha kwenye ligi kilimshawishi kocha wa timu ya taifa ya Denmark kumpa nafasi katika mechi mbili za kirafiki dhidi ya Sweden na Finland mechi ambazo Denmark ilishinda. Katika mechi zote hizo, Okare alicheza vizuri katika beki ya kati kwa kuhakikisha mashambulizi ya wapinzani yanapozwa yasimfikie golikipa.


Alex Oxlade-Chamberlain (England, 18)

Kwa wanaofuatilia soka la England wanamjua vizuri kijana huyu anaichezea klabu ya Arsenal. Licha ya kuwa na umri mdogo, Chamberlain ana uwezo mkubwa na anaonekana kukomaa kiuchezaji.

Katika mechi 18 za ligi kuu England na nne za ligi ya mabingwa alizocheza, Chamberlain alionesha kiwango kizuri kiasi cha kumshawishi kocha Roy Hodgson kumjumuisha katika kikosi cha England. Mchezaji huyu ambaye ameichezea timu ya taifa ya wakubwa mechi moja tu dhidi ya Norway anatarajiwa na wengi kuwa ataonesha kiwango kikubwa katika fainali za mwaka huu.


Jetro Willems (Netherlands, 18)


Mlinzi wa kushoto ambaye msimu uliopita ndio ulikuwa wa kwanza kwake kucheza katika kikosi cha kwanza cha PSV Eindhoven. Kujumuishwa kwake katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kunatokana na majeruhi ya mchezaji mwenzake wa PSV Erik Pieters.

Willems amecheza mechi moja tu ya kimatifa dhidi ya Bulgaria katika mechi ya kirafiki kujiandaa na fainali za mwaka huu. Sasa kinda huyu atakuwa na hamu ya kucheza mechi yake ya pili wakati Uholanzi itakapocheza mechi yake ya kwanza ya mashindano haya dhidi ya Denmark. Kama Jetro Willems atacheza mechi hiyo, basi ataweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji mdogo kuliko wote kuwahi kucheza katika historia ya fainali hizo. Rekodi ya sasa bado inashikiliwa na Enzo Scifo ambaye alicheza mechi akiwa na miaka 18 na siku 115.


Rafal Wolski (Poland, 19)

Kinda huyu anayecheza nafasi ya kiungo anasemekana kuwa ndiye mchezaji mwenye kipaji kuwahi kutokea Poland kuliko wote. Wolski atakuwa anatamani kung'aa katika fainali hizo kama atapewa nafasi.

Wolski amekuwa akiichezea Legia Warszawa kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba mashabiki wa timu hiyo wanamfananisha na kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya
Borussia Dortmund Mario Götze. Timu mbalimbali kubwa zimeanza kumnyemelea mchezaji huyu na haitakuwa ajabu kuona mchezaji huyo akiihama Legia Warszawa baada ya fainali hizi.

AddThis Social Bookmark Button

 
Ukame wamalizika... Dakika 1,541, saa 26 bila bao kwa Torres
Written by Mwandishi Spoti    Friday, 23 March 2012 07:10   

Fernando TorresWIKI iliyopita mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres alimaliza ukame wa kutofunga mabao, ikiwa ni baada ya kucheza dakika 1,541 bila kufumania nyavu.

Torres alimaliza ukame huo, baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Leicester City katika Kombe la FA.

Japo Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao 5-2, vyombo vyingi vya habari vilitawala habari ya Torres kufunga.

Wakati Torres alipofunga goli la kwanza, mashabiki wa Chelsea waliibuka kwa furaha kubwa. Wachezaji wenzake walimkimbilia na kumkumbatia kama vile wanamfurahia mchezaji kinda aliyefunga goli katika mchezo wake wa kwanza.

Kumbe El Nino alikuwa amefunga goli lake la kwanza baada ya dakika 1,541

Torres aliigharimu Chelsea pauni milioni 50 na anapokea mshahara unaokaribia pauni milioni 175,000 kwa wiki. Hii inaonesha ni mchezaji wa kiwango

AddThis Social Bookmark Button

Read more...
 
Juma Nature kafanya nichukie Wabongo
Written by Laurent Samatta    Thursday, 08 March 2012 09:25   

Christine John 'Sintah'KUNA tabia ambazo mtu zinaweza kukufanya ukachukia kitu fulani, hadi kikasababisha pia kukuletea madhara.

Vipo vitu vingi ambavyo mtu unaweza ukavichukia, kama vile kutopenda wanaume au wanawake wenye umbo kubwa, warefu, weupe, kutopenda chakula fulani, kuligana na roho yako inataka nini.

Jina la mwanadada Christine John 'Sintah', si geni katika masikio ya wadau wa filamu hasa wale wanaopenda kazi za wasanii wa Bongo.

Sintah alijizolea umaarufu mkubwa pindi alipokuwa akitoka kimapenzi na msanii wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature, miaka kadhaa iliyopita, ambapo kwa sasa anatoka na Wazungu.

ALIVYOANZA SANAA

Akifanya mahojiano maalumu na mwandishi wa makala haya, Sintah, anasema kuwa alianza kujihusisha na filamu mwaka 2002 akiwa katika kundi la Kaole, ambapo alidumu hapo kwa muda wa miaka miwili.

Anasema baada ya harakati zake za kutafuta jina na fedha alipata kazi Clouds Radio ikiwa ni mwaka 2003 na baada ya hapo akaamua kwenda chuo nchini Uganda mwaka 2005 hadi 2007.

Sintah anasema baada ya kurudi kutoka huko akarudi upya kwenye game na kucheza filamu mbili ambazo ni 'Alama ya X' na 'Jasusi'.

CHANGAMOTO ALIZOPITIA
Sintah anasema kuwa hakupitia changamoto nyingi katika kazi yake kwani kipaji chake ndicho kilichokuwa kinazungumza katika kila kitu alichokuwa anafanya.

Anasema wakati huo alikuwa ni mdogo umbo pamoja na sura yake vilikuwa na mvuto wa hali ya juu, lakini hata hivyo hakuweza kupoteza usichana wake kwa kutembea na wasanii ambao tayari walikuwa wana majina.

AddThis Social Bookmark Button

Read more...