Arsenal yamwambia RVP: 'huendi popote'
Thursday, 19 July 2012 05:10   

KWA mujibu wa mtandaoo wa Goal.com, Arsenal inajiandaa kumwambia mshambulaiji wa timu hiyo Robin Van Persie kuwa hataruhusiwa kuondoka katika usajili unaoendelea sasa.

Inaaminika kuwa mshambulaiji huyo raia wa Uholanzi atashikilia msimamo wake wa kutaka kuhama Arsenal wakati atakapokutana tena na Arsene Wenger pamoja na mtendaji mkuu Ivan Gazidis kwa ajili ya mazungumzo upya.

Lakini baadhi ya maofisa wa Arsenal wametonya kuwa klabu hiyo iko tayari kumpoteza bure mchezaji huyo kuliko kumwacha aondoke sahivi.

Hatua hiyo ya Arsenal kumng'ang'ania Van Persie inaonekana na watu wengi ni kama vile kumkomoa mshambuliaji huyo.

Arsenal wanajua kuwa Van Persie atafikisha miaka 30 ifikapo oktaba 2013 na amekuwa akikabiliwa na majeruhi mara kwa mara. Hivyo Arsenal wanaona kuwa huenda timu ambazo zinamvizia sahivi zisimvizie tena mwakani.

"Hatutamruhusu Van Persie kuondoka na tutahakikisha kuwa anamalizia mkataba wake. Atakapofikisha miaka 30, hakuna timu ambayo itakuwa tayari kumlipa mshahara mkubwa. Hivyo itakuwa rahisi kusaini mkataba mpya." Kilisema chanzo kimoja cha karibu na Arsenal.

Arsenal inatarajiwa kusafiri na Van Persie siku ya Jumamosi kwenda Kuala Lumpur, Malaysia kucheza mechi tatu za kiarafiki ambapo moja kati ya mechi hizo itakuwa dhidi ya Manchester City.

AddThis Social Bookmark Button

 
Ibrahimovic atua rasmi PSG
Thursday, 19 July 2012 05:01   

MKURUGENZI wa michezo wa Paris Saint-Germain Leonardo amethibitisha kuwa mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic tayari ameshamalizana na PSG

Wakala wa mshambuliaji huyo alikuwepo nchini Ufaransa siku chache zilizopita akijaribu kukamilisha dili la kumpeleka mteja wake katika klabu hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Ibrahimovic atakuwa akilipwa Euro milioni 13 kwa mwaka huku gharama iliyotumika kumuhamisha Ibrahimovic kutoka AC Milan kwenda PSG ikikadiriwa kuwa ni Euro milioni 23.

"Tumeshafikia makubaliano na Ibrahimovic. Kuanzia sasa Ibrahimovic ni mchezaji wa PSG." Alisema Leonardo siku ya Jumanne usiku.

Wakala wa Ibrahimovic Mino Raiola akiongea katika makao makuu ya timu hiyo siku ya Jumanne usiku alisema: "Kila mmoja ana furaha kwa kukamilika dili hili."

PSG ilitarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari jana huku lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kumtambulisha Ibrahimovic pamoja na kiungo Marco Verratti.

AddThis Social Bookmark Button

 
Chelsea yagomewa
Thursday, 19 July 2012 04:51   

KOCHA wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine Mircea Lucescu amesema kuwa klabu yake imeikataa ofa ya pauni milioni 25 kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji William.

Kiungo huyo raia wa Brazili amekuwa akiwindwa na Chelsea toka mwezi Januari, na kocha wake amewahi kukiri kuwa watamruhusu kuondoka kwa bei sahihi.

"Nimemwambia William kuwa anaweza kuondoka lakini kama tutapokea ofa sahihi. Willium ni mchezaji mzuri sana." Alisema Lucescu.

Lucescu alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa William ni mchezaji mzuri zaidi ya Hazard na kuhoji iweje Chelsea itoe pesa nyingi kwa ajili ya Hazard lakini itoe pesa ndogo kwa ajili ya Willium wakati William ni bora zaidi ya Hazard.

"Waliilipa Lille pesa nyingi kwa ajili ya Hazard lakini hawapo tayari kulipa pesa nyingi kwa ajili ya William ambaye kwangu mimi ni bora zaidi ya Hazard." Alisema kocha huyo.

AddThis Social Bookmark Button

 
AVB avimbisha kichwa
Thursday, 19 July 2012 04:46   

KOCHA wa Tottenham Hotspur Andre Villas-Boas yupo tayari kuwapiku Chelsea na kumsajili mshambuliaji wa Porto Hulk

Hulk aliwasili London siku ya Jumanne akiandamana na timu ya taifa ya Brazili itakayoshiriki mashindano ya Olympiki.

Villas-Boas, ambaye amewahi kufanya kazi na Hulk wakati akiifundisha Porto anataka kutumia pesa nyingi kumsajili mchezaji huyo na tayari amekwishapewa ruhusa ya kuanza mazungumzo na mchezaji huyo.

Mshambuliaji huyo mwenye nguvu alitarajiwa kujiunga na Chelsea, lakini dili hilo linaonekana kukaribia kufa baada ya Porto kutaka walipwe euro milioni 38 ili kumwachia mchezaji huyo.

Baada ya Chelsea kusitasita kutoa kiasi hicho cha pesa, Tottenham Hotspur imeamua kuingia katika mbio za kumwania mchezaji huyo huku ikiamini kuwa inaweza kuishawishi Tottenham kushusha kiasi hicho cha hela.

AddThis Social Bookmark Button

 
West Ham kumnasa Maiga
Monday, 16 July 2012 10:39   

Klabu ya West Ham ya ligi kuu nchini England ipo katika hatua za mwisho kumnasa mshambuliaji Modibo Maiga kwa pauni milioni 4 kutoka Sochaux.

Maiga raia wa Mali alikaribia kujiunga na Newcastle january mwaka huu kabla ya dili hilo kuharibika kutokana na mshambuliaji huyo kugundulika ana majeraha ya goti.

Sam Allardyce ambaye ni kocha wa West Ham yupo katika harakati za kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kabla ya msimu ujao kuanza.

Kocha huyo pia amekuwa akiwawinda mshambuliaji kutoka Norwich, Grant Holt na Yannick Sagbo kutoka klabu ya Evian.

AddThis Social Bookmark Button

 
  • «
  •  Start 
  •  Prev 
  •  1 
  •  2 
  •  3 
  •  4 
  •  5 
  •  6 
  •  7 
  •  8 
  •  9 
  •  10 
  •  Next 
  •  End 
  • »


Page 1 of 17