Yanga yatete kombe la Kagame
Monday, 30 July 2012 10:40   

MABAO yaliyofungwa na Hamis Kiiza na Said Bahanuzi yameipa ubingwa wa mara tano Yanga wa Kombe la Kagame.

Kwa ushindi huo Yanga ambao walikuwa mabingwa watetezi wamefanikiwa kutetea ubingwa wao, huo kwa mara nyingine tena.

Mchezo huo ambao ulitawaliwa na vituko vingi kabla ya kuanza nahodha wa Azam, Agrey Morris alikataa kupeana mikono na mwenzake wa Yanga, Nadir Haroub.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku Azam wakionekana kutaka kupata bao la mapema, ambapo iliwachukua dakika mbili kabla ya John Boko kulifikia lango la Yanga lakini alipiga shuti lilotoka nje.

Dakika 12 baadae, Kipre Tchetche kama angekuwa makini angeweza kuipatia Azam bao la kuongoza.

Azam waliendelea kulisakama lango la Yanga ambapo dakika ya 15 walipata kona iliyopigwa na Abubakar Salum na kuungwanishwa na Moris kwa kichwa na mpira kumgonga Ally Mustapha.

Yanga walijibu shambulizi hilo kwa Haruna Niyonzima kuwalamba chenga mabeki wa Yanga na kupiga krosi safi iliyookolewa kiufundi na Deogratius Munishi.

Baada ya kuona mashambulizi yamezidi kocha wa Yanga, Tom Sainttief alimuita Niyonzima na kumweleza kitu ambapo baada ya hapo ‘alijiungashusha’ na kujidai ameaumia huku kocha huyo akitumia muda huo kuwaita wengine na kuwapa maelekezo.

Azam walitawala kabisa mchezo huo kwa dakika 30 za mwanzo huku wenzao wa Yanga wakipoteana kabisa.

Dakika 30 Bahanuzi alifanikiwa kuwalamba chenga mabeki wa Azam ndani ya eneo la hatari lakini alitoa pasi ambayo ilitoka nje.

Rashid Gumbo alipiga shuti kali dakika ya 34 ambalo lilitemwa na Munishi na kumkuta Bahanuzi ambaye alipiga nje.

Uzembe uliofanywa na Agrey Moris kwa kumudishia mpira mfupi Munishi ambao uliwahiwa na Kiiza aliyepiga shuti na kumgonga kipa na kujaa wavuni.

Kipindi cha pili kilianza kwa David Luhende kuwalamba chenga wachezaji wa Azam na kumpa pasi safi Gumbo ambaye alipiga shuti lilodakwa na Munishi.

Yanga ambao walionekana kupata nguvu zaidi kipindi cha pili, waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao.

Kama Kiiza na Niyonzima wangekuwa makini wangeweza kuipatia Yanga mabao dakika za 58, 82 na 86.

Mabeki wa Azam watajutia makoa waliyofanya katika mchezo huo ambapo walitegeana kuokoa mpira ambao uliwahiwa na Bahanuzi na kuachia shuti kali lilojaa wavuni na kuipatia Yanga bao la pili.

Kikosi: Ally Mustapha, Nadir Haroub, Stephano Mwasika, Kelvin Yondani, David Luhende, Athuman Iddy, Rashid Gumbo/Juma Seif, Oscar Joshua, Hamis Kiiza, Said Bahanuzi na Haruna Niyonzima.

Azam FC: Deogratiu Munishi, Ibrahim Shikanda, Said Morad, Erasto Nyoni, Aggey Moris, Jabir Aziz/George Odhiambo, Kipre Tchetche/Mrisho Ngasa, Salum Abukar, John Boko, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhani Chombo.

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, alisema kikosi chake kimecheza vizuri huku akitoa sifa nyingi kwa kiungo wake chipukizi Abubakar Salum.

Alisema kikosi hicho hakitabadilika katika ligi kuu msimu ujao na kuwaongezea mazoezi kwa ajili ya ligi hiyo.

Pia aliongeza kuwa John Boko ameshindwa kufanya vile ambavyo alitegemea baada ya kucheza katika kiwango cha chini.

Alisema kupoteza mchezo huo kumetokana na kutotumia nafasi ambazo walipata huku wapinzani wao wakizitumia.

Kwa upande wake kocha wa Yanga alisema Tom Saintfiet alisema anashukuru ameanza vizuri katika timu hiyo kwa kunyakuwa kombe la kwanza.

Alisema timu ya Azam ni kati ya timu bora ambayo ina viungo wengi wazuri, ambapo kama itatunzwa itakuja kuwa bora zaidi baadae kutokana na kuwa na wachezaji wengi vijana.

Alisema anawashukuru wachezaji wake kwa kufuata maagizo yake japokuwa ailikuwa katika kipindi kifupi toka alipojiunga na timu hiyo.

Wakati huo huo Said Bhanuzibaliyesajiliwa na timu hiyo alitokea Yanga amefanikiwa kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga mabao sita.

Kutokana na kunyakuwa ubingwa huo Yanga imefanikiwa kupata kitita cha dola 30,000, Azam walioshika nafasi ya pili wamepata dola 20,000 huku Vita ya Kongo DRC iliyoshika ya tatu ikipata dola 10,000.

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji alionekana ntu mwenye furaha kubwa kuliko mwingine yoyote katika matokeo hayo.

Manji ambaye aliapa ataifanyia kweli Azam kabla ya mchezo huo, alionekana mwenye furaha kubwa wakati wote huku akicheza wakati mwingi wa mchezo.

“Achana na Manji, yaani kama kuna kitu kimemfurahisha ni leo,” alisema shabiki mmoja.

Naye mshambuliaji Said Bahanuzi, aliwakosha zaidi mashabiki wa Yanga kutokana na kufunga bao hilo katika dakika za nyongeza.

AddThis Social Bookmark Button

 
Mashabiki Azam wamuhoji Ngasa
Monday, 30 July 2012 10:21   

MASHABIKI wa Azam wamesema, wanataka mchezaji wa timu hiyo Mrisho Ngasa awaombe radhi kwa kitendo cha kuwafuata mashabiki wa Yanga na kuvaa jezi yao, anaripoti Hamisi Miraji.

Hiyo ilitokea kwenye mchezo wa nusu fainali kati ya Azam na Vita, ambapo lambalamba ilishinda mabao 2-1 katika mchezo wa Kombe la Kagame.

Katka mchezo huo, Ngasa aliifungia timu yake bao safi na la ushindi na kushangilia bao hilo kwa kuwafuata mashabiki wa Yanga na kwenda kuwapa mikono.

Wakizungumza na Spoti Starehe jana, mashabiki hao walisema wamesikitishwa na kitendo cha mchezaji huyo kwa kushangilia bao lake na kuwafuata mashabiki wa Yanga kuwapa mkono.

Walisema, kubwa zaidi kilichowauma mashabiki hao baada ya mchezo huo kumalizika, mchezaji huyo alikwenda kuwafauta mashabiki wa Yanga na kuvaa jezi ya timu hiyo.

Mmoja wa mashabiki wa timu hiyo, Mussa Chito alisema, kitendo alichofanya mchezaji huyo kimewaumiza na kuwapa fedheha kubwa.

Kitendo kile kimetuuma sana sisi mashabiki na kimetutia fedhea kutokana kuonesha waziwazi mchezaji huyo kuwa na mapenzi na Yanga,” alisema.

Mashabiki hao walisema, kama kweli mchezaji huyo hana mapenzi na Yanga anatakiwa awaombe radhi mashabiki wa Azam ili kuiweka mioyo yao safi.

Walisema, bila ya kufanya hivyo watapoteza imani na mchezaji huyo katika kuitumikia klabu ya Azam jambo ambalo litakuwa sio zuri.

AddThis Social Bookmark Button

 
AS Vita yatwaa nafasi ya tatu
Monday, 30 July 2012 10:06   

TIMU ya AS vita ya Congo imefanikiwa kunyakuwa nafasi ya tatu ya kombe la Kagame, baada ya kuifunga APR ya Rwanda kwa magoli 2-1.

Mechi hiyo iliyoanza saa saba kamili mchana, ilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta goli la mapema.

Iliwachukua Vita dakika 12 kufanya shambulizi la maana langoni mwa APR, ambapo mshambuliaji wa timu hiyo Mutombo Kazadi, alishindwa kumalizia krosi nzuri ya Niemba Nkanu.

Vita ambayo imesifika kwa kucheza kandanda la chini katika mashindano ya mwaka huu, iliendelea kulisakama lango la APR ambapo katika dakika ya 18 mshambuliaji wa timu hiyo Magola Mapanda aliipatia bao la kwanza kwa shuti kali.

Timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini hadi kipindi cha kwanza kinaisha AS Vita ilikuwa ikiongoza kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza huku APR wakionekana kutaka kusawazisha huku wapinzania wao wakitafuta la kuongeza.

Dakika ya 68 mshambuliaji hatari wa timu hiyo Mutombo Kazidi alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la pili na kukatisha matumaini ya APR kupata nafasi ya tatu.

Baada ya kufungwa bao hilo APR walionekana kutokata na kuendelea kulisakama lango la wapinzani wao.

wakati mpira ukielekea kumalizika, APR walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi baada ya mchezaji wake Mugiraneza Jean kufunga goli katika dakika ya 89 kwa shuti kali.

Hadi mwamuzi wa mchezo huo, Antony Ogwayo, kutoka Kenya anapuliza kipenga cha mwisho, AS vita ilitoka kifua mbele kwa mabao 2-1 na hivyo kukamata nafasi ya tatu katika mashindano ya Kagame.

AddThis Social Bookmark Button

 
Simba, Azam kuuana leo
Tuesday, 24 July 2012 05:57   

Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Simba leo itakuwa na kibarua kigumu pale itakapokabiliana na wanalambalamba Azam FC katika robo fainali ya mwisho ya michuano ya Kagame.

Mechi hiyo ambayo itaanza saa kumi za jioni itatanguliwa na robo fainali nyingine kati ya Atletico ya Burundi na AS Vita ya Jamuhuri ya Congo. Mechi ya Atletico na AS Vita itaanza saa nane mchana.

Mchezo kati ya Simba na Azam unatarajiwa kuwa mkali sana haswa kwa kuwa timu hizo zimekuwa zikikamiana kwa siku za hivi karibbuni.

 

AddThis Social Bookmark Button

 
Nizar Khalfan aapa
Tuesday, 24 July 2012 05:45   

MCHEZAJI mpya wa Yanga, Nizar Khalfan amesema, hakuna timu yoyote itakayowasimamisha katika mashindano hayo mpaka hatua ya fainali na kuchukuwa ubinwa.

Akizungumza na Spoti Starehe juzi mara tu baada mchezo wao na APR ya Rwanda kumalizika, alisema timu yao imecheza vizuri na imetimia kila idara kwa hiyo hakuna wa kuwazuia.

“Timu yetu ipo vizuri sana imetimia kila sekta ina wachezaji wazuri na wenye vipaji vya kucheza mpira mi sidhani kama kuna timu ya kutusimamisha kila mtu aliona jinsi tunavyocheza,” alisema.

Nizar alisema, wachezaji wa Yanga sasa hivi wameelewana jinsi ya kuucheza mpira na hasa wanapokuwa uwanjani kutokana na kufundishwa mbinu mbalimbali na mwalimu wao.

Mchezaji huyo aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nchin Canada katika timu ya White Camp Vancouver alikisifu kikosi cha APR na kusema ni kizuri.

Yanga imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kagame baada ya kufanikiwa kuwaondosha Mafunzo kwa Changamoto ya penati na sasa itakabiliana na APR katika mchezo wa nusu fainali hapo kesho.

 

AddThis Social Bookmark Button

 
  • «
  •  Start 
  •  Prev 
  •  1 
  •  2 
  •  3 
  •  4 
  •  5 
  •  6 
  •  7 
  •  8 
  •  9 
  •  10 
  •  Next 
  •  End 
  • »


Page 1 of 13