Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano Mil. 200 kuzibomoa Simba, Yanga
Mil. 200 kuzibomoa Simba, Yanga PDF Print E-mail
Written by Christian Hall   
Thursday, 13 May 2010 06:09

Na Erasto Stanslaus

KLABU inayokuja kwa kasi katika soka la bongo, Azam FC imetenga kitita cha sh. milioni 200 kwa lengo la kuimarisha kikosi chake katika msimu ujao.



Azam ambayo imepanda daraja misimu miwili iliyopita imekuwa moja ya timu inayotimiza malengo yake inayojiwekea baada ya kumaliza Ligi Kuu ikiwa katika nafasi ya tatu.

Lengo la kwanza la Azam lilikuwa kubaki katika Ligi Kuu msimu wake wa kwanza wakati lengo la pili kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi nne za juu na wamefanikiwa sasa wanamalengo ya kutwaa taji hilo msimu ujao.

Katika kutimiza malengo hayo msimu ujao timu hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya SSB Ltd imetenga pesa hizo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.

Azam ambao tayari wameanza mazungumzo ya baadhi ya wachezaji ambao wenyewe wameonesha nia ya kuvaa jezi za timu hiyo msimu ujao kutokana na dau kubwa waliotangaziwa.

Kwa mujibu wa mmoja wa kiongozi wa timu hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake kwani yeye si msemaji wa timu hiyo alisema kitita hicho tayari kimeanza kufanya kazi kwa kupata wachezeaji tegemeo wa timu hizo.

Kiongozi huyo alisema kitita hicho kimefanikiwa kumnasa beki wa kutumainiwa wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kwa kumwagia sh. milioni 40 sambamba na mshambuliaji wake Mrisho Ngassa ambaye wamemwaahidi kumpa milioni 45.

Ofa hizo za Azam pia zimeamnasa mshambuliaji wa Yanga, Mkenya Boniface Ambani ambaye alitofautiana na Kocha wake Kostadin Papic katika maslahi ya usajili wake mpya.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa mazungumzo baina yao na wachezaji hao wamefikia katika nafasi nzuri na wote wamekubali kuichezea timu hiyo na kilichobaki na uongozi kukamilisha taratibu za uhamisho.

"Hakuna mchezaji mwenye akili ambaye atakuwa tayari kuiacha ofa hiyo eti kwa sababu ya jina la timu anayochezea, Bosi amekubali kutoa pesa hizo baada ya kuona mafanikio ya miaka miwili katika ligi hiyo," alisema kiongozi huyo.

Chanzo hicho kiliendelea kupasha kuwa sasa ofa hiyo imemgeukia kiungo wa Simba, Ramadhani Chombo 'Ridondo' ambaye naye ametengewa dau kubwa.

"Tumesikia Chombo anatakiwa na Hodood lakini tunaamini kuwa hawezi kulikataa dau ambalo tumemwekea, lazima atatua tu kwetu," alisema kiongozi huyo.

Wachezaji ambao tayari wamemwaga wino katika klabu hiyo ni Jackson Chove na mshambuliaji kutoka Polisi ya Uganda.

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday127
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week127
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month878
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15309

We have: 3 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.87
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.