Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano Yanga hatarini kubomoka
Yanga hatarini kubomoka PDF Print E-mail
Written by Christian Hall   
Thursday, 06 May 2010 04:39

* Papic ahaha kuwadhibiti

Na Erasto Stanslaus

WAKATI Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic 'Clinton' akiwa katika mikakati ya kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, tayari baadhi ya timu zipo katika mchakato wa kukibomoa kikosi hicho.

Papic ambaye amesitisha likizo yake kwa lengo la kukamilisha usajili, tayari ametangaza wachezaji anaowatema ikiwa pamoja na wale anawaowania katika kikosi chake.

Mserbia huyo ametangaza kuwamwaga wachezaji tisa huku wakitaka kusajili sita ambao wazawa ni wawili na wakigeni wanne.

Wakati Papic akiwa katika mchakato huo, timu za Azam tayari imekamilisha mpango wa kumng'oa katika kikosi hicho beki wake kati, Nadir Haroub 'Canavaro'.

Mbali na Canavaro lakini Maafande wa Rwanda timu ya APR nao wapo katika mazungumzo na kumnasa mshambuliaji wa kutumainiwa na timu hiyo, Mrisho Ngassa na wameamuahidi donge nono zaidi wanaotoa Yanga.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka katika uongozi wa Azam, kilisema kuwa tayari wamezungumza na Canavaro na kumuahidi donge nono ambalo mwenyewe amekubaliana nalo.

"Canavaro msimu ujao anatua Azam kwani tayari mwenyewe ameridhia kuichezea timu hiyo na sasa kilichobaki ni kuongeza na klabu yake ambayo tunaamini tutamalizana nao," kilisema chanzo hicho chenye ukaribu na Canavaro.

Kwa upande wa Ngassa, ujumbe mzito wa APR umetua nchini kwa lengo la kufanya mazungumzo na mshambuliaji huyo ambaye anaonekana kukubaliana na dau walilomtangazia.

Ngassa ambaye amekiri kuzungumza na Maafande hao alisema kwa sasa anamkataba na Yanga hivyo kama klabu hiyo ikimalizana na Yanga yupo tayari kuondoka.

Papic alisema lengo lake ni kuwa na kikosi imara msimu ujao hivyo mbali na wachezaji aliotangaza kuwatema hatakubali kumwachia mchezaji yoyote katika kikosi chake.

"Nimekuta wachezaji wamesajiliwa lakini kwa wale niliokubali kiwango chao nataka kuendelea nao na moja ya mikakati yangu ni kuwaongezea mshahara pamoja na pesa za usajili ambazo zilikuwa ndogo tofauti na uwezo wao," alisema Papic.

Papic aliongeza: "Nimepunguza kiwango cha pesa kwa wageni ambao hawakuwa na msaada katika kikosi hicho lakini pesa hizo zitatumika kwa wazawa, wakiwemo hao wanaotakiwa hivyo wasibabaike na hizo timu".

Kocha huyo mwenye asili ya Serbia alisema viwango vya wachezaji hao si vya kucheza tena katika timu za hapa nyumbani badala yake waangalie soka la kulipwa.

Naye msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema wachezaji wote wanaotakiwa na timu hizo wanamikataba na Yanga hivyo wanaweza kuwapata wachezaji hao kama wakiwa tayari kuvunja mikataba yao.

 

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday127
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week127
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month878
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15309

We have: 3 guests, 1 bots online
Your IP: : 38.107.191.85
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.