Sunday 05th of September 2010
| Chelsea yawagonganisha Ferguson ,Benitez |
|
|
|
| Written by Christian Hall |
| Monday, 03 May 2010 04:01 |
|
LONDON, Uingereza KOCHA wa Manchester United na mwenzie wa Liverpool Rafa Benitez wamejikuta katika mzozo uliosababishwa na ratiba ya mechi zao za mwisho msimu katika Ligi Kuu ya nchini hapa. Fergie amekasirishwa na kitendo cha Chelsea kukutana na Liverpool ikiwa ni siku tatu tu baada ya Liverpool kuchapwa na Atletico Madrid katika nusu fainali ya Ligi ya Europa. Kocha huyo anahisi Liverpool itakuwa na uchovu wa mechi na hivyo kuipa nafasi Chelsea kushinda kirahisi. Na kocha wa Anfield Benitez amesema Manchester United iko katika nafasi nzuri ya kutwaa taji kwa kuwa mechi yao itachezwa baada ya mechi ya Chelsea. Hali hiyo inamfanya kocha huyo ahisi United itakuwa tayari imeshajua matokeo ya Chelsea huko Anfield. Benitez alisema "Nashangaa, Hispania mechi mbili za mwisho kwa timu zote huchezwa kwa wakati mmoja. "Kwa hali hiyo kila mtu atakuwa katika nafasi ile ile. "Lakini hapa ni tofauti, kila mtu anajua nini kitatokea." Chelsea inaongoza ligi hiyo kwa pointi moja nyuma ya United huku kukiwa na mechi mbili mkononi, ushindi wao huko Anfield utaifanya United kucheza kufa na kupona ili kushinda huko Sunderland. Fergie alisema "Kucheza mchana baada ya kucheza Alhamisi si uungwana kwa timu za England. "Inatokea mara nyingi sana, inatokea kwetu na kwa wengine, hatuwezi kuwa na ratiba iliyobanana kiasi cha kushindwa kuipa timu mapumziko. "Wamecheza kwa dakika 90 Alhamisi kila siku nasema hazipati msaada mkubwa zinapokuwa katika michuano ya Ulaya. "Kwa hiyo mnakuwa mnawategemea wachezaji." |
| Last Updated on Monday, 03 May 2010 04:03 |






![]() | Today | 126 |
![]() | Yesterday | 211 |
![]() | This week | 126 |
![]() | Last week | 1478 |
![]() | This month | 877 |
![]() | Last month | 8325 |
![]() | All days | 15308 |
We have: 3 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.85
,
Today: September 05, 2010
Your IP: : 38.107.191.85
,
Today: September 05, 2010
Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.









