Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano Manji kufanya kufuru
Manji kufanya kufuru PDF Print E-mail
Written by Christian Hall   
Thursday, 29 April 2010 05:59

Na Erasto Stanslaus


*Wabongo kuula msimu ujao

 

BAADA ya Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa Yanga, Yusuph Manji kumaliza tofauti zake na Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Kostadin Papic maarufu kama Clinton, ameahidi kuishushia neema klabu hiyo.

Manji ambaye iliripotiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na Papic hali iliyomfanya kocha huyo kutishia kuibwaga timu hiyo kutokana na kunyanyaswa na Mjumbe huyo.

Kutokana na hali hiyo, Manji alikutana na Papic na kujadili mambo mbalimbali juu ya mkataba wake na hatimaye kukubaliana na Papic ataendelea kuinoa timu hiyo kwa mafanikio zaidi.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka katika ofisi ya Mjumbe huyo, Manji sasa ameahidi kusajili wachezaji wapya sita ikiwa wageni wawili na wazawa wanne.

Mbali ya ahadi hiyo ya usajili pia Manji ameahidi kuwaongezea maslahi wachezaji wazawa kutokana na umuhimu wao walioonesha katika msimu huu.

"Manji ameamua kuwaongezea mkataba mnono wachezaji wa Kitanzania baada ya kugundua kuwa wageni waliosajiliwa walishindwa kuisaidia timu na badala yake wazawa kuwa ndio sehemu ya mafanikio ya timu hiyo," kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilisema kuwa Manji ameahidi kusajili wageni wapya wawili wakigeni kwa mujibu wa matakwa ya Papic, kwa ghalama yoyote ikiwa pamoja na kuwaongeza wanne ambao wamependekezwa na kocha huyo.

Papic ambaye anatarajia kwenda likizo baada ya kuwapa likizo wachezaji wake hadi Julai tayari kwa kujiandaa na msimu ujao huku akiwa ameshapendekeza majina ya wachezaji anaowaacha na wale anawaataka.

Wachezaji waliotemwa tayari na Papic ni Steven Bengo, Boniface Ambani, Moses Odhiambo, Kabongo Honore, George Owino, Robert Jama Mba na Wisdom Ndhlovu wakati wazawa ni Hamis Yusuph na Ali Msigwa.

Chanzo hicho kilisema majina ya wachezaji wa Tanzania watakaoongezwa katika kikosi cha Papic tayari yamewasilishwa katika ofisi hiyo huku wale wa kigeni watakuwa kati ya wanaofanyiwa majaribio.

wachezaji wa kigeni wanaofanya majaribio na Yanga ni Waghana Isack Boakye, Keneth Asamoah na Osai Boakye na Sylvester Selapj Mokaine wa Afrika Kusini.


 

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday125
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week125
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month876
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15307

We have: 4 guests, 3 bots online
Your IP: : 38.107.191.88
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.