Kombe la United Super lasogezwa
Written by Mwandishi Spoti    Tuesday, 24 July 2012 05:08   

KAMATI ya mashindano ya Kombe la United Super imesogeza mbele tarehe ya mashindano hayo hadi Julai 29 badala ya Julai 25, mwaka huu.

Kamati hiyo imeamua kusogeza mbele tarehe ya mashindano hayo ambayo awali yalikuwa yafanyike Julai 25 baada ya timu shiriki kuomba ili wachezaji wengi waliokuwepo nje ya Dar waweze kurejea.

Mratibu wa mashindano hayo, Yahya Abrahmani Mwinyi 'Batigo' amesema tarehe ya mashindano hayo imesogezwa mbele baada ya timu shiriki kuomba kwa ajili ya wachezaji wao waliopa safarini kurejea.

"Katika kikao chetu tuliamua mashindano hayo yarushwe kwa siku nne mbele kwani timu nyingi ambazo zilipaswa zianze tarehe ya awali kuomba yasogezwe mbele,” alisema.

Mratibu huyo alisema, katika kikao hicho cha kamati yao ya  mashindano kilipanga makundi ya mashindano hayo.

AddThis Social Bookmark Button

 

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote