Sunday 05th of September 2010
|
Written by Erasto Stanslaus
|
|
Saturday, 24 July 2010 15:51 |
|
Jeshi la Yanga hatari Na Julius Kihampa KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Kostadin Papic ametangaza jeshi lake la askari 27 litakalopigania ubingwa wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara. Jeshi hilo litakuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha wanarudisha taji lao la ubingwa walilopokwa msimu uliopita na watani wao wa jadi, Simba. Msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema wamesajili wachezaji 27 ambao walikuwa wakitakiwa na kocha wao mara baada ya kumaliza kwa msimu uliopita. Kwa idadi hiyo ya wachezaji Yanga imewazidi wapinzani wake wa jadi, Simba kwa mchezaji mmoja kwani wao wamesajili wachezaji 26.
Sendeu alitaja wachezaji hao kuwa ni makipa Ivan Knezevic, Yaw Berko na Nelson Kimath wakati walinzi ni Shadrack Nsajigwa, Salum Telela, Stephano Mwasika, Nadir Haroub 'Cannavaro', Isaack Boakye, Mohamed Mbegu, Chacha Marwa, Ibrahim Job na Fred Mbuna. Viungo ni Ernest Boakye, Nurdin Bakari, Godfrey Bonniface, Athuman Idd 'Chuji', Kigi Makasi, Abdi Kassim, Shamte Ally, Razack Khalfan na Omega Sunday Seme. Washambuliaji ni Jerry Tegete, Idd Mbaga, Nsa Job, Kenneth Asamoah na Yahaya Tembo. Kwa kikosi hicho Yanga itakuwa imewatema kipa aliyezoea kukaa benchi, Steven Marashi, beki wa Malawi, Wisdom Ndhlovu, Ali Msigwa, Robert Jama Mba na John Njoroge. Alisema usajili waliofanya wamezingatia kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara ikiwa pamoja na michuano ya Kimataifa. "Kwa mujibu wa Papic, kikosi alichosajili ni kizuri na hana wasiwasi nacho katika michuano hiyo iliyoko mbele yetu," alisema Sendeu. Sendeu alisema baada ya kumaliza suala la usajili kwa sasa wameanza mazoezi wakiwa na kikosi kamili cha timu hiyo kinachojindaa na ligi hiyo. Katika hatua nyingine, Sendeu alisema uongozi umemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Emmanuel Mpangala kuwa Meneja wa muda wa timu hiyo. |
Powered by Business Times Ltd
Valid XHTML and CSS.