Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano ?Mtoto wa Papic aiua Simba SC
?Mtoto wa Papic aiua Simba SC PDF Print E-mail
Written by Erasto Stanslaus   
Saturday, 24 July 2010 15:49

Na Mohamed Akida

UJIO wa mtoto wa Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic, Todor umeongeza hali ya ushindi kwa timu ya Yanga dhidi ya Simba kutokana na mtoto huyo kumshinikiza baba yake kushinda mechi hiyo.

Yanga itavaana na Simba, Agosti 14 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Agosti 21.

Todor aliliambia Spoti Starehe, juzi mazoezini kuwa furaha yake ni kuona Simba inafungwa na hilo anaamini litafanikiwa kutokana na baba yake kujua mapenzi yake yapo wapi.

“Baba anajua ni jinsi gani nisivyoipenda rangi nyekundu na nashukuru baba anafundisha timu yenye rangi za njano na kijani,” alisema Todor.

Todor ambaye pia ni mshabiki wa timu ya Tiafa ya Ghana aliongeza: “Naweza nikawepo katika mchezo wao, na najua baba lazima atafanya kitu ili wshinde iwe kama zawadi yangu kuja mtembelea na hufanya hivyo kila ninapokwenda”.

Mtoto huyo alisema ijapokuwa timu ya Taifa ya Serbia nayo inatumia jezi za rangi nyekundu lakini kwa upande wa klabu anavutiwa na rangi ya njano na kijani kutokana na muonekana wake.

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday125
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week125
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month876
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15307

We have: 3 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.87
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.