Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano ?Joto la Simba, Yanga laanza kupanda
?Joto la Simba, Yanga laanza kupanda PDF Print E-mail
Written by Erasto Stanslaus   
Saturday, 24 July 2010 15:45

Na Chausiku Omary

JOTO la mchezo wa watani wa jadi wa Simba na Yanga limeanza kupanda baada ya wachezaji wa timu hizo kuanza kutambiana kuibuka na ushindi.

Miamba hiyo itakutana katika mchezo wa kwanza wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Agosti 14 ikiwa ni ufunguzi wa pazia la msimu wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Agosti 21.

Simba na Yanga watakutana tena katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo katika mzunguko wa kwanza Oktoba 16.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji nyota wa timu hizo wameanza tambo kwa kila mmoja akimtambia mwenzie kuwa ataibuka na ushindi katika mchezo huo.

Beki mpya wa kushoto wa Yanga, Stephano Mwasika alisema haoni sababu ya kupoteza mchezo huo ambao ni muhimu kwao ikiwa ni dira ya msimu huu.

“Kutokana na kikosi tulichosajili na mafundisho ya kocha wetu Kostadin Papic, naamini tutashinda mchezo huo, na kujiweka vizuri kwa msimu ujao ambao naamini tutakuwa mabingwa,” alisema Mwasika.

Kipa namba moja wa Simba, Juma Kaseja anaamini mchezo huo utakuwa mgumu lakini hawana hofu ya kupoteza mchezo huo kwani hakuna mabadiliko makubwa yatakayoifanya waupoteze mchezo huo.

“Yanga naona ni wale wale hakuna jipya sana ambalo litatutia hofu katika mchezo huo, ushindi kwetu ni tabia yetu, tutawafunga hakuna shaka katika hilo,” alisema Kaseja.

Mimba hiyo ya Simba na Yanga ipo katika mazoezi makali ya kujiandaa na msimu ujao.

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday127
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week127
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month878
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15309

We have: 4 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.88
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.