Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano Mafisango kuleta 'suprise' Azam
Mafisango kuleta 'suprise' Azam PDF Print E-mail
Written by Erasto Stanslaus   
Saturday, 24 July 2010 15:44

Na Mohamed Akida.

MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Azam FC, Mutesa Mafisango atafanya kile ambacho watu hawakutarajia na hawakuwahi kukiona katika Ligi Kuu Bara katika msimu iliyopita na kuwataka mashabiki wa Azam kusubiri waone.

Mafisango amesajiliwa na Azam msimu huu akitokea katika timu ya APR ya Rwanda ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda.

Akizungumza wakati wa mazoezini na Azam, mafisngo alisema kwa sasa hawezi kutoa ahadi yoyote kwa amashabiki na uongozi wa timu hiyo lakini atakapokuwa uwanjani anatoa suprise ambayo hawajawahi kuiona.

Mafisango amesema amefurahi kucheza Tanzania kutokana na ligi hiyo kuwa na ushindani mkubwa tofauti na ile ya kwao ambayo ushindani wake ni mdogo sana.

Mafisango ndiyo anakamilisha idadi ya wachezaji watano wa kulipwa katika kikosi cha Azam ambacho kesho kinatarajia kwenda kuweka kambi Visiwani Zanzibari kwa ajili ya kujiandaa na ligi hiyo itakayoanza Agosti 21.

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday127
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week127
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month878
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15309

We have: 4 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.89
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.