|
AVB avimbisha kichwa |
|
Thursday, 19 July 2012 04:46 |
|
|
KOCHA wa Tottenham Hotspur Andre Villas-Boas yupo tayari kuwapiku Chelsea na kumsajili mshambuliaji wa Porto Hulk
Hulk aliwasili London siku ya Jumanne akiandamana na timu ya taifa ya Brazili itakayoshiriki mashindano ya Olympiki.
Villas-Boas, ambaye amewahi kufanya kazi na Hulk wakati akiifundisha Porto anataka kutumia pesa nyingi kumsajili mchezaji huyo na tayari amekwishapewa ruhusa ya kuanza mazungumzo na mchezaji huyo.
Mshambuliaji huyo mwenye nguvu alitarajiwa kujiunga na Chelsea, lakini dili hilo linaonekana kukaribia kufa baada ya Porto kutaka walipwe euro milioni 38 ili kumwachia mchezaji huyo.
Baada ya Chelsea kusitasita kutoa kiasi hicho cha pesa, Tottenham Hotspur imeamua kuingia katika mbio za kumwania mchezaji huyo huku ikiamini kuwa inaweza kuishawishi Tottenham kushusha kiasi hicho cha hela.
|