Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano Topland, Shoko wang'ara Pool
Topland, Shoko wang'ara Pool PDF Print E-mail
Written by Erasto Stanslaus   
Saturday, 24 July 2010 15:42

Na Erasto Stanslaus

TIMU za Topland na Shoko zimeonesha matumaini ya kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Safari Lager Pool Championship ngazi ya mkoa wa Kinondoni.

Michuano hiyo ambayo ilianza Julai 22 katika mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Moro na Kagera, ambapo kwa Kinondoni inachezwa katika Bar ya Meeda, Sinza.

Shoko hadi sasa wanaongoza katika kundi A baada ya kushinda michezo yake miwili iliyocheza kati ya Meeda na Bahama Mama, wakati nafasi ya pili katika kundi hilo inashikwa na Meeda iliyotandika Jaba.

Katika kundi B, timu inayoongoza ni Topland iliyozichapa timu za Vatcan na Madrid katika michezo yao ya juzi na jana na Vatcan inashika nafasi ya pili katika kundi hilo baada ya kuifunga 4ways.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Pool wilaya ya Kinondoni (KIPA), Zahor Lijalu, leo kwa Kinondoni watakuwa wamepata timu zitakazoingia hatua ya robo fainali zitakazopigwa Agosti 6 na nusu fainali itachezwa Agosti 7 na fainali itakuwa sikukuu ya nanenane.

Mashindano hayo ya mkoa yatatoa timu ya mkoa huo ambao itashiriki mashindano ya Safari lager Pool ngazi ya Taifa yatakayofanyika Septemba 15 hadi 19 mkoani Arusha.

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday130
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week130
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month881
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15312

We have: 3 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.88
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.