Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano Man United yambakisha Rooney
Man United yambakisha Rooney PDF Print E-mail
Written by Erasto Stanslaus   
Saturday, 24 July 2010 15:41

MANCHESTER, Uingereza

MKURUGENZI wa Manchester United, David Gill, atakutana na Wayne Rooney, kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuongeza katika klabu hiyo.

Wakati nyota huyo kabakisha miaka miwili katika mkataba wake, uongozi wa United, umepanga kumuongezea mkataba mchezaji huyo.

Juzi, United, ilitangaza kukubaliana na Nemanja Vidic, kubaki klabuni hapo kufuatia taarifa kuwa angeweza kuhamia Real Madrid au AC Milan.

Rooney, atafanya mazungumzo na United baada ya kurejea mapumzikoni na atakuwa mchezaji wa pili kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

"Mpango wa sasa ni kukutana na Wayne na washauri wake pindi atakaporudi likizo kwa lengo la kuzungumzia mkataba mpya,” Gill, aliwaambia waandishi wa habari.

"Aliwahi kusema na sisi tuliwahi kusema kuwa, tunahitaji kukutana na kulizungumzia suala hili, ili tuendelee kumpa maisha mapya hapa United.

"Ukiangalia malengo yake na jinsi anavyojituma katika klabu hii ni wazi mpango huu utafanikiwa."?

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday126
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week126
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month877
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15308

We have: 3 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.87
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.