Sunday 05th of September 2010

Home Mawasiliano Toure: Niliitosa Man United
Toure: Niliitosa Man United PDF Print E-mail
Written by Erasto Stanslaus   
Saturday, 24 July 2010 15:40

MANCHESTER, Uingereza

NYOTA mpya wa Manchester City, Yaya Toure, amefichua siri kuwa, Manchester United ilitaka kumsajili msimu uliopita lakini aliitolea nje. 

Kiungo huyo mwenye thamani ya pauni milioni 24, alisema alikuwa na nafasi ya kuihama Barcelona msimu uliopita baada ya kuisaidia timu hiyo kuichapa United, katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Alisema "mwaka jana, Manchester United, ilikuwa ikinitaka, wakati nilipokuwa naongelea kuhusu kuongeza mkataba wangu, United, iliniuliza kama napenda kujiunga nayo.

"Manchester United, ni klabu kubwa duniani, lakini City, imekuwa ndiyo changamoto yangu."

Toure, aliamua kubaki Nou Camp, badala ya kuhamia Old Trafford.

Lakini miezi 12 baadaye, alihusishwa kuhamia Eastlands ambako sasa atakuwa anaongoza kwa mshahara katika ligi hiyo, atakuwa akilipwa pauni 180,000 kwa wiki.

Alisisitiza kuwa, City, ndiyo changamoto yake kubwa sambamba na kucheza pamoja na kaka yake   brother.

Toure, kwa sasa yuko New York na City kwa ajili ya ziara ya kimichezo, aliongeza "nilitaka kucheza na kaka yangu siku moja, lakini suala si pesa."

 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday130
mod_vvisit_counterYesterday211
mod_vvisit_counterThis week130
mod_vvisit_counterLast week1478
mod_vvisit_counterThis month881
mod_vvisit_counterLast month8325
mod_vvisit_counterAll days15312

We have: 3 guests, 2 bots online
Your IP: : 38.107.191.86
 , 
Today: September 05, 2010

Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.