AVB kuibomoa Chelsea
Monday, 09 July 2012 08:01   

BAADA ya kuthibitishwa kuwa kocha mpya wa Tottenham Hotspur na kuahidiwa fungu nono la usajili, kocha Andre Villas-Boas anajiandaa kuivamia Chelsea na kuwasajili Raul Meireles na Daniel Sturridge.

Andre Villas-Boas ambaye alitimuliwa na Chelsea miezi michache iliyopita, alikuwa rafiki mkubwa wa Meireles na ndiye aliyemtoa Liverpool kwenda Chelsea. Kocha huyo pia alionesha imani kubwa kwa Sturridge kwa kumpanga kila mechi.

Baada ya kufanikiwa kumnasa Gylfi Sigurdsson aliyekuwa akisakwa pia na Liverpool, sasa AVB anajiandaa kutumia kiasi cha pauni milioni 100 za usajili atakazopewa kuhakikisha anawanasa Meireles na Sturridge.

Jermaie Deffoe ndie mshambuliaji pekee aliyesalia katika kikosi cha Tottenham Hotspur na huku dili ya kumchukua moja kwa moja Emmanuel Adebayor likionekana kugonga mwamba, kocha AVB anataka kumsajili Sturridge ili kusaidiana na Defoe.

Majaliwa ya kiungo Luka Modric ndani ya klabu hiyo bado hayajawa wazi huku mchezaji huyo akiwa tayari ameiomba klabu yake hiyo kuondoka.

Kocha Andre Villas-Boas ameanza kujiandaa kwa maisha bila Modric kwa kupanga kumsajili Meireles kuziba pengo litakaloachwa wazi na Modric.

AddThis Social Bookmark Button

 

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote