Van Persie kutosaini Arsenal
Thursday, 05 July 2012 15:01   

Mshambuliaji tegemeo wa Arsenal Robin Van Persie ameweka wazi nia yake ya kutoongeza mkataba na klabu hiyo ya London.

Mkataba wa Van Persie na Arsenal unaisha mwishoni mwa msimu ujao (2013) na ingawa Arsenal imempa ofa ya mkataba mpya, Van Persie ameamua kutosaini mkataba huo mpya.

Arsenal ilifanya mazungumzo bila mafanikio na Van Persie juu ya mkataba mpya siku chache kabla mshambuliaji huyo hajaenda kuungana na wenzake katika timu ya taifa ya Uholanzi kwa ajili ya fainali za EURo 2012.

Pande hizo mbili zilikubaliana kuliacha suala hilo na kwamba wangezungumza tena baada ya fainali za Euro 2012 kuisha, lakini siku chache kabla Arsenal hawajajikusanya kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, Van Persie ameamua kutoongeza mkataba wake na Arsenal

"Nimefikiria sana na kwa muda mrefu, lakini nimeamua kutoongeza mkataba wangu na Arsenal." Aliandika Van Persie katika ukurasa wake wa twitter.

Baada ya Van Persie kutoa uamuzi wake, klabu ya Arsenal ilitoa taarifa yake ikisema kuwa inaheshimu maamuzi ya Van Persie na inatumaini Van Persie ataendelea kuwa mtiifu kwa Arsenal na kuitumikia Arsenal kwa muda uliobaki

Licha ya taarifa hiyo ya Arsenal ambayo inaonesha kuwa Arsenal wako tayari kumbakisha mshambuliaji huyo na kumwachia aondoke bure msimu ujao, wadadisi mbalimbali wa soka wanaona kuwa Van Persie atauzwa huku Manchester City ikiwa inaongoza kumwania mshambuliaji huyo.

Hata hivyo inasemekana Arsenal haiko tayari kuendelea kuinufaisha Manchester City na huenda wakamuza Juventus, PSG au Real Madrid.

AddThis Social Bookmark Button

 

Maoni 

  1. #1 thomas
    2012-08-2205:20:58 kaondoka ajui anacho kwenda kukifanya zaidi ya kuuwa kiwango,na wenger tumia akili zaidi tafuta mabeki wazuri sana
  2. #2 vetto
    2012-12-0310:32:28 wenger jitahid kusajili wachezaji wenye uzoef

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote