|
Balotelli aiangamiza Ujerumani |
|
Friday, 29 June 2012 04:52 |
|
|
Mshambuliaji mwenye sifa ya utukutu Mario Balotelli usiku wa kuamkia leo alikuwa shujaa wa Italia baada ya kuifungia timu hiyo magoli mawili katika ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ujerumani.
Kwa matokeo hayo Italia sasa itacheza dhidi ya Hispania katika fainali ya kombe la Euro 2012 siku ya Jumapili.
Balotelli alifunga goli la kwanza kwa kichwa katika dakika ya 20 baada ya kumzidi ujanja beki wa ujerumani Holger Badstuber na kuunganisha krosi ya Antonio Cassano.
Katika dakika ya 36, Balotelli aliwanyanyua tena vitini mashabiki wa Italia baada ya kutumia vizuri pasi ndefu ya Ricardo Montolivo ambayo mabeki wa kati wa Ujerumani walishindwa kuicheza na kumkuta Balotelli aliyoituliza vizuri kisha kupiga shuti kali la mbali lililomwacha golikipa wa Ujerumani Manuel Neur akiangalia tu asijue la kufanya.
Ujerumani walipata goli la kufutia machozi katika dakika ya 92 lililofungwa na Mesut Ozil kwa njia ya penati baada ya beki mmoja wa Italia kuunawa mpira ndani ya 18.
|