Rooney ndani ya bifu na Capello
Thursday, 28 June 2012 05:36   

BAADA ya England kutolewa na Italia katika mchezao wa robo fainali ya fainali za Euro 2012, kumetokea bifu kali ya maneno kati ya mshambuliaji wa timu hiyo Wyne Rooney na kocha wa zamani wa England, Fabio Capello.

Rooney ndiyo aliyoanza chokochoko hiyo ya maneno kwa kusema kuwa wachezaji wa timu hiyo walikuwa hawamuelewi wala kuelewa maelekezo ya kifundi waliyokuwa wanapewa na Capello.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United alisema kuwa wachezaji wa timu hiyo wameelewa kiurahisi mbinu na maelekezo ya kocha wa sasa Roy Hodgson kuliko ilivyokuwa kwa Capello kwa kuwa hakuna matatizo ya mawasiliano tena

Maneno hayo ya Rooney yalionekana kumkasirisha sana Capello ambaye alimjibu Rooney kwa kusema kuwa mshambuliaji huyo anaelewa maelekezo ya kiufundi anayopewa na bosi wake wa manchester United Alex Ferguson pekee na si kocha mwingine.

Akihojiwa na gazeti la Corriere dello Sport, Capello alisema: "Baada ya kuangalia mechi kati ya England na Italia, nadhani Rooney anaelewa lugha ya Kiskochi pekee"

Capello alisema hivyo akimaanisha lugha mama ya kocha wa Manchester United Alex Ferguson ambaye ni raia wa Scotland.

Toka England itolewe na Italia katika hatua ya robo fainali ya Euro 2012, mshambuliaji wa timu hiyo Wyne Rooney amekuwa akitupiwa lawama na watu tofauti kutokana na kiwango kibovu alichokionesha siku hiyo.

AddThis Social Bookmark Button

 

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote