|
Sheringham aipa nafasi England |
|
Monday, 04 June 2012 14:33 |
|
|

MSHAMBULIAJI wa zamani wa England, Tedy Sheringham anaamini timu hiyo inaweza kuwashangaza watu katika fainali za Kombe la Mataifa Ulaya, iwapo kocha Roy Hodgson atacheza karata zake vizuri.
Sheringham anaona kocha huyo, anaweza kuiongoza England kupata mafanikio katika fainali hizo na anaamini mchanganyiko wa wachezaji vijana na wale wenye uzoefu utakuwa ni silaha muhimu kwake.
Sheringham ambaye aliifungia England mabao 11 katika michezo 51, alisema mechi ya jana dhidi ya Ubelgiji itakuwa kipimo sahihi kwao.
"Siamini kama tulicheza vizuri dhidi ya Norway, lakini wachezaji walikuwa wanaelewa nini ambacho kocha alikuwa anakihitaji."
Sheringham anakiri kukosekana kwa Frank Lampard na Gareth Barry katika fainali hizo ni pigo kubwa katika sehemu ya kiungo.
|