Bundi azidi kumwandama Jack Wilshere
Monday, 21 May 2012 11:33   

 

Jack Wilshere BALAA limezidi kumuandamwa mchezaji wa Arsenal, Jack Wilshere     baada ya habari kuzagaa kuwa atahitaji kufanyiwa operesheni ndogo katika goti lake. Mchezaji huyo atasafiri kwenda Sweden kwa ajili ya matibabu zaidi ya goti lake.

Wilshere, 20, aliukosa msimu mzima uliopita kutokana na majeruhi ya kiwiko cha mguu. Majeraha hayo yalimfanya afanyiwe operesheni na ilisemekana kuwa angekuwa fiti mwezi wa pili, lakini alipata majeraha mapya ambayo yalimweka nje msimu mzima.

Taarifa kutoka klabu ya Arsenal ilisema: "matibabu ya Jack wilshere, yamekuwa yakiendelea taratibu. Hivyo Wilshere atasafiri kwenda Sweden kumuona daktari kwa ajili ya matibabu zaidi."

Kulikuwa na taarifa kuwa Wilshere atashiriki katika mashindano ya Olympiki, lakini taarifa hizi mpya zinatia mashaka kama Wilshere, ataweza kuiwakilisha Uingereza katika mashindano hayo.

 

AddThis Social Bookmark Button

 

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote