| Man Utd yabaniwa na Everton | |
|
|
Katika mchezo huo ulioisha kwa wageni Everton kuchomoa magoli yote yaliyofungwa na kufanya matokeo kuwa 4-4. Pointi 2 walizopoteza leo zinafanya msimamo kuonyesha Manchester wana pointi 83 na mahasimu wao Manchester City wakiwa na pointi 77 wakiwa na mchezo mmoja ambao wanacheza na Wolves ugenini leo. Tofauti ya pointi 3 itakayotokea kama Manchester City atashinda, itafanya mchezo wao wa Aprili 30 pale Etihad uwe wa muhimu sana kwa kila timu kwa sababu inawezekana ndio utakaoamua mshindi. Everton ilianza kuongoza mchezo huo kwa goli la Jelavic dakika ya 34 kabla ya Wayne Rooney kuisawazishia Man Utd dakika ya 41. Goli alilofunga Rooney limemfanya afikie rekodi ya wafungaji bora wa timu hiyo akishika nafasi ya nne sawa na Dennis Violett na George Best wote wakiwa na magoli 179. Kipindi cha pili Manchester walikuja na kasi na kufanikiwa kupata magoli mawili ya haraka kupitia kwa Welbeck (dakika ya 57) baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Valencia akipasiana na Carrick na goli la tatu lilifungwa na Nani (dakika ya 61). Dakika ya 67 Fellaini aliifungia timu yake goli la pili kabla ya Rooney tena dakika ya 69 kufunga goli la la pili kwake na la 4 katika mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 4-2. Kwa goli hili Rooney akawaacha wenzie kwenye magoli 179 akawa na magoli 180 akiwa nyuma ya wakali Denis Law, Bobby Charlton na Jack Rowley katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote klabuni hapo. Zikiwa zimebakia dakika 7 tu mchezo kumalizika na Man Utd wakiwa tayari wameridhika na matokeo ya 4-2 Everton walizitumia dakika hizo chache kupiga goli mbili za haraka katika dakika za 83 (Jelavic) na 85 (Pienaar)!
|
Mbio za kuwania ubingwa zimeingia dosari baada bya Manchester United kushindwa kuibuka na ushindi muhimu ilipocheza na Everton katika uwanja wa Old Trafford.
