| Barcelona hoi kwa Madrid | |
|
|
Mechi hiyo ya upinzani wa jadi maarufu kama El Classico inakuwa ni kama kulipiza kisasi kwa timu ya Real Madrid ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikishindwa kuifunga Barcelona hasa baada ya kuwasili kwa Maurinho. Dakika ya 15 tu ya mchezo Madrid walipata goli la kwanza kupitia kwa Sami Khedira aliyefunga kutokana na makosa yaliyofanywa na golikipa wa Barcelona Victor Valdes. Goli hilo lilidimu hadi dakika ya 70 ya mchezo baada ya Alexis Sanchez kufunga goli la kusawazisha. Wakati kelele za wenyeji katika dimba lao la Nou Camp zikizidi kurindima kwa furaha ya kusawazisha, dakika takribani 3 tu baadaye Cristiano Ronaldo alifunga goli zafi la ushindi dakika ya 73. Sasa Madrid wako mbele kwa pointi 7 huku kila timu ikiwa imebakiza michezo minne tu. Kipigo cha jana kinakuwa ni cha pili kwa Barcelona baada ya majuzi tu kufungwa 1-0 na Chelsea nchini Uingereza katika pambano la nusu fainali la kombe la klabu bingwa Ulaya. Critiano Ronaldo anazidi kupaa kwenye chati ya ufungaji magoli nchini humo baada ya sasa kufikisha magoli 42 na kuifanya klabu hiyo kuwa na jumla ya magoli 109 msimu huu pekee ambayo ni rekodi mpya. Timu zote sasa zinahamishia mawazo yao katika michuano ya klabu bingwa baada ya kuwa na matokeo mabaya katika mechi za awali zilizochezwa ugenini. Real Madrid ilifungwa 2-1 ilipocheza na Bayern Munich nchini Ujerumani. |
Klabu ya Barcelona sasa inaweza kuwa imepoteza matumaini ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu Hispania maarufu kama La Liga baada ya jana kukubali kichapo kutoka kwa Real Madrid.
