Man City waangusha pointi 2
Saturday, 31 March 2012 20:31   

Manchester City vs SunderlandHaijawahi tokea timu ya Sundeland ikashinda mechi katika uwanja wa Etihad unaomilikiwa na Manchester City.

Na leo nusura wavunje rekodi hiyo baada ya kuongoza kwa magoli 3-1 mpaka dakika ya 85 kabla ya Man City kufunga magoli mawili ya haraka haraka dakika ndani ya dakika moja.

Sunderland walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za City katika dakika ya 31 kwa goli la Sebastian Larsson ambalo lilisawazishwa na Baloteli kwa mpira wa penati.

Bao hilo liliwachanganya zaidi wachezaji wa City na mchezaji Baloteli alianza mchezo wa kujiangusha angusha katika eneo la hatari la Sunderland katika janja ya kumdanganya mwamuzi awape penati juhudi ambazi zilizaa matunda dakika ya 43 kwa City kupata goli kwa penati baada ya Edin Dzeko kuchezewa faulo, penati iliyofungwa na Baloteli.

Wakionekana kujiamini hasa baada ya kuifunga City katika mchezo wa kwanza kwa goli 1-0, Sunderland walipata bao la pili kwa mpira wa kichwa wa Nicklas Bendtner katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.

Larsson aliandika bao la tatu dakika ya 55 na kuzidisha simanzi kwa mashabiki wa City na kuzidi kufifisha matumaini ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

City walihitaji shujaa wa kuwaokoa na Mancini alimtoa Silva na kumpa nafasi Tevez.

Zikiwa zimebakia dakika tano tu za muda wa kawaida, Baloteli aliichambua ngome ya Sunderland na kufunga goli la 2 dakika ya 85 na baada tu ya Sunderland kuanzisha mpira katikati City walifanya ambacho kilionekana hakitawezekana baada ya Kolarov kufunga goli la kusawazisha dakika ya 86!

Sasa City wako nyuma ya vinara Manchester United kwa pointi 2 ambao watacheza mchezo wao Jumatatu ugenini kwa Blackburn Rovers na kama wakishinda wataongeza tofauti hiyo hadi pointi 5.

Baloteli ameifungia timu yake magoli hayo mawili ikiwa ni siku chache baada ya kocha huyo kutamka kuwa hana imani na Baloteli

 

 

 

AddThis Social Bookmark Button

 

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote