| Barcelona, AC Milan hakuna mbabe | |
|
|
AC Milan ndiyo waliokuwa kwenye dimba lao la nyumbani la San Siro. Wageni Barcelona walikuwa na nafasi ya kufunga kama penati waliyokuwa wakiilalamikia kwa mchezaji Alexis Sanchez ingetolewa. AC Milan walipata nafasi ya wazi mwanzoni kabisa mwa mchezo lakini Robinho alishindwa kulenga goli kwa kupiga mpira juu ya goli. Sasa mabingwa watetezi Barcelona watatakiwa washinde mechi ya marudiano itakayochezwa wiki ijayo katika dimba lao la Nou Camp ili wajihakikishie nafasi ya kucheza nusu fainali dhidi ya mshindi kati ya Chelsea na Benfica. AC Milan wanaoongoza msimamo wa ligi ya Italia, Serie A, wameendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika mechi za robo fainali katika uwanja wa nyumbani. |
Timu za AC Milan na BArcelona zimeshindwa kufungana katika mechi ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
