Maajabu ya namba za Messi
Friday, 23 March 2012 06:26   

KILA mmoja kwa sasa anamtaja Lionel Messi, kwani mchezaji huyu anaonekana ni mwiba haswa katika mambo ya upachikaji mabao.

Wakati Barcelona ilipotoa kipigo cha mabao 7-1 na Bayer Leverkusen, mashabiki wakaanza kumchimbua na kutaka kujua huyu ni nani haswa.
Kuna mengi unaweza kumzungumzia Messi, lakini hapa tunajaribu kutazama maajabu za namba zinazomuhusu mchezaji huyo.

2: Ni idadi ya hat-trick alizopiga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye msimu mmoja.

3: Hii ni idadi ya hat-trick alizopiga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufikia rekodi iliyowekwa na  Filippo Inzaghi. Pia Messi amefanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tatu huku akiwa na miaka 24 tu. Sasa Messi amefikia rekodi ya Michel Platini, Johan Cruyff na Marco Van Basten ya kuchukua tuzo hiyo mara tatu.

4: Ameibuka mfungaji bora katika Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo na sasa yuko mbioni kuibuka mfungaji bora kwa mara ya nne. Mchezaji pekee aliyewahi kuibuka mfungaji bora mara nne ni shujaa wa zamani wa Bayern Munich, Gerd Muller.

5: Idadi ya mabao aliyofunga katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Pia amekuwa mchezaji wa kwanza wa Barcelona kufunga mabao matano katika mechi moja tokea alipofanya hivyo Zaldua mwaka 1965.

6: Amefunga mabao katika mashindano sita tofauti mwaka huu. Mashindano hayo ni La Liga, Kombe la Mfalme, Spanish Supercopa, UEFA supercup, Kombe la Dunia na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa kufanya hivyo Messi amefikia rekodi ya mchezaji mwenzake Pedro aliyoiweka mwaka 2009.

12: Mpaka sasa amefunga mabao 12 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuifikia rekodi ya Ruud Van Nistelrooy aliyoiweka mwaka 2002-2003. Messi ana zaidi ya mechi moja za Ligi ya Mabingwa kuweza kuweka rekodi mpya.

18: Toka aichezea Barcelona kwa mara ya kwanza mwaka 2005, Messi amefanikiwa kubeba vikombe 18 na Barcelona.

22: Baada ya kufunga hat-trick katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Uswisi wiki chache zilizopita, Messi sasa ameshafungia Argentina mabao 22 katika mechi 67.

24: Ameweka rekodi kwa kufunga mabao 24 katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

49: Mshambuliaji huyo wa Barcelona amefanikiwa kufunga mabao 49 katika Ligi ya Mabingwa akiwapita Alessandro Del Piero (44), Filippo Inzaghi (46), Eusebio (47), Andriy Shevchenko (48). Magoli yake matano aliyoyafunga dhidi ya Leverkusen yamemfanya  amfikie Alfredo Di Stefano katika nafasi ya nne ya wafungaji bora katika Ligi ya Mabingwa nyuma ya Thierry Henry (51), Van Nistelrooy (54) na Raul (71).

54: Amefunga mabao 54 msimu uliopita katika mashindano yote akilingana na Cristiano Ronaldo.

93: Amefanikiwa kutoa pasi za mabao 93 kwa timu yake ya Barcelona. 73 katika misimu minne iliyopita na 20 msimu huu mpaka sasa.

188: Toka Pep Guardiola alipokabidhiwa jukumu la kuinoa Barcelona, Messi amefunga  mabao 188 katika mechi 201 za mashindano.

228: Ni jumla ya mabao aliyofunga Messi katika timu ya Barcelona akiwa pungufu mabao saba tu kuweza kufikia rekodi ya mfungaji bora wa Barcelona wa muda wote Cesar Rodriguez aliyefunga mabao 235.

AddThis Social Bookmark Button

 

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote