Niyonzima hawezi kukwepa lawama
Thursday, 15 March 2012 09:07   

NAJUA watu wengi huwa hawapendi kusema ukweli na hasa pale inapotokea ukweli unauma ua hautaki useme kwa kuwa tu huyu ni kipenzi cha watu.

Lakini kwangu hili ni lazima niliseme hata kama wanajangwani wote watanipiga basi wafanye hivyo, maana na yenyewe kufuga ugonjwa mwisho wake ni kifo.

Ni ukweli usiopingika kuwa Yanga mara nyingi huwa inafungwa na Azam maarufu kama wanatamutamu,lakini hii mechi ya mwishoni mwa wiki iliyopita, historia ingeweza kubadilika na Yanga kushinda.

Makosa yaliyofanywa na mchezaji wa kimataifa wa Rwanda Haruna Nyozimana wenyewe wanamwita 'Fabregas' ni ya kitoto na ya kipuuzi ambayo kwa heshima na hadhi aliyonayo anafaa kuitwa mhaini.
Mchezaji anayecheza mchangani ndio anatakiwa afanye kitendo kama hicho. Haruna dakika ya 11 tu ya mchezo anapewa kadi ya njano kwa kosa la kipuuzi kabisa la kumfundisha kazi mwamuzi, hazipiti dakika tano Haruna anaomba kadi nyingine tena kwa kulazimisha  pamoja na kwamba refa alikwenda mbali zaidi ili kuepuka kumpa kadi nyingine mchezaji huyo.

Lakini wapi haikusaidia, alimfuata hadi kati ya uwanja na kumshambulia kwa lugha ambayo watazamaji wote tulijua tu kuwa huyu kadi nyekundu anaitaka mwenyewe.

Upo uwezekano Haruna Niyonzima amelewa sifa na kujiona yeye ndio Yanga na Yanga ndio yeye, jambo ambalo nadhani anajidanganya.

Walikuwepo kina Sunday Manara  au Computer wako wapi? Na Yanga bado ipo,lakini inavyoelekea hata benchi la ufundi linaloongozwa na Mserbia Papic na mzawa Fredy Minziro nalo liko chini ya mchezaji huyo wa kimataifa.

Sikumwona hata kocha mmoja kukemea kwa kitendo chake cha kupewa kadi ya kwanza tu ya njano na badala yake walisubiri kuungana naye kupinga kadi ile ya pili, ambayo mchezaji huyo dhahiri kabisa aliitaka kwa sababu anazozijua yeye.

Mchezaji huyo Nyozimna bado ameendelea kuteka mawazo hadi ya wachezaji wenzake kukubali kuanzisha vurugu ya kijinga bila kumlaumu mchezaji huyo, ambaye kadi aliitaka mwenyewe kwa tukio la yeye na Agrey Morris kufanyiana purukushani tena mbali kabisa na maeneo ya hatari yasiyo na madhara kwa kona au penalti.

Wachezaji wenye upeo hawakutakiwa kabisa kumuunga mchezaji huyo wakati alikuwa akifanya 'maamuzi' ya kuigharimu timu na kuwafanya wenyewe wafanye kazi ya kuziba pengo lake.

Uongozi wa Yanga umekaa kimya bila kutoa tamko kali kwa mchezaji huyo wa kimataifa na yupo nchini kama mchezaji wa kulipwa na akilipwa mamilioni ya pesa akifanya upuuzi huo.

Ningekuwa mimi ni Mwenyekiti wa Yanga, Llyod Nchunga, ningemkata mshahara wa miezi mitatu. Lazima angewajibika katika hilo ili iwe fundisho kwa wachezaji wa aina yake.

Niyonzima amefanya kitendo ambacho kwa mtu wa mpira bila kujali ushabiki, ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa  matokeo ya pale uwanjani,ikwa ni pamoja na kufanya watu kupigwa mabomu ya machozi, hadi kupelekea kifo cha kijana mmoja shabiki na polisi kufanya kazi ya ziada kwa sababu ya mtu mmoja tu tena anatoka nje ya nchi yetu.

Nadhani imefika wakati viongozi wetu wa klabu pamoja na makocha makawajenga wachezaji wetu kuheshimu matokeo ya uwanjani na kuwaacha mashabiki na viongozi ndio watoe 'maamuzi' baada ya dakika 90.

Kitendo walichofanya Yanga si cha kiuungwana na kwa watu kama sisi wapenda amani ni fedheha kubwa mno kwa timu kubwa kama hiyo, kwa wenzetu walioendelea ilikuwa ni sehemu tosha kabisa ya watu kujiuzulu kwa tukio hilo.

Wito kwa wachezaji ni kufanya kazi moja tu ya kucheza mpira na kuwafurahisha mashabiki wenu, kazi ya uamuzi sio yenu wako watu wamesomea na wamebobea na huyo refa aliyepigwa Israel Nkongo, ni juzi tu ametoka kuchezesha mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa maana ndio kazi yake na anaijua vizuri.

Haruna Nyozimana amejipunguzia sifa kwa watu wenye kupenda mpira ambao kwetu sisi wengine ushabiki ni mwiko, tunaangalia hali halisi kwangu mimi Nyozimana ni msaliti namba moja wengine wanafuatia.

AddThis Social Bookmark Button

 

Maoni 

  1. #1 Ahuman
    2012-03-1510:40:03 Uandishi wako wote umejaa mapenzi tu. kwani Niyonzima kutoka nje ndio aonewe bila sababu? Kuchezesha mechi za nje sio ishu ila hapa Nkongo alikuwa na ajenda yake ya siri kama walikuwa wanafanya purukushani na Agrey Moris kwa nini kadi apewe niyonzima peke yake. Kama una ushahidi mtu alukufa katika vurugu za yanga katoe ushahidi polisi acha utoto
  2. #2 Alfred myalla
    2012-03-1607:46:48 Huyo mwaisabula ni mbaguzi sana,anambagua niyonzima kwa kuwa anatoka Rwanda na sio mtanzania,anapo teza sifa ya kuwa mwanaspoti mzalendo na mwalimu,ushabik i wake ndio umetawala maoni yake anapaswa kuongea kwa kutumia mantiki kwa hali ya mchezo ulivyokuwa.Niyonzima ni mchezaji mzuri na anayejiheshimu wala hajajipunguzia sifa alichokuwa akifanya na kujitetea kutokana na uchezeshaji mbovu wa huyo mwamuzi wake wa FIFA.Klabu ya yanga hipo imara dhidi ya hujuma zozote kwa klabu yao.tunamuomba mwaisabula haachane na Yanga na wachezaji wake kwani haimuusu.
  3. #3 Alfred myalla
    2012-03-1608:02:08 Pia nawaomba wahusika katika gazeti hili wasiwape nafasi ya kutoa maoni ya kukera na kuhudhikama haya, yaliyotolewa na mwaisabula watu wote wanaongelea yanga tu pasipo kuangalia upande wa mwamuzi na maudhui nzima ya mchezo ule namuunga mkono Ahuman na pia maamuzi ya wazee wa yanga dhidi ya uhamuzi wa TFF Yanga oyeeeeeee
  4. #4 john peter
    2012-04-0221:21:49 imetokea misri na watu wamekufa,sababu ya upumbavu wenu. Niyonzima amecheza vzr mnawatuma mabeki wenu wapuuzi, wasiojua mpira kumchezea rafu, halafu iweje mtabaki hapo hapo na fitna zenu, siwalaumu chamazi ndio tabia zao uhuni tu na kununua marefa hamna lolote,mlimdang anya ngasa west ham. nunueni mpaka wakina mwaisabula njaa inawasumbua,taf uteni sio kuirukia yanga tu.maisha bila yanga inawezekana.tuachieni yanga yetu ya kamati yenu iliyojaa viongozi wa simba,
  5. #5 john peter
    2012-04-0221:23:13 kamati ya simba inaendesha ligi

Tuma maoni

Maoni yenye kukera, kutukana na kuvunja sheria za nchi yatafutwa

:D:lol::-);-)8):-|:-*:oops::sad::cry::o:-?:-x:eek::zzz:P:roll::sigh:
Bold Italic Underlined List Quote